"Oolisikia wapi?" KRG ampasha Alex Mathenge kwa kusema maceleb ni maskini

Muhtasari

• Krg alimjibu Mathenge kwamba wakati wengine wanatafuta pesa yeye ako anaendelea kupiga umbeya.

KRG the Don na Alex Mathenge
KRG the Don na Alex Mathenge
Image: Instagram

Msanii KRG the Don ameamua kuzima moto kwa kutumia moto na kumtuma mwizi kumshika mwizi.

Kupitia kwa instastories zake, msanii huyu ameshindwa kukimya na kumjibu mchekeshaji Alex Mathenge kuhusu madai yake juzi kati aliposema kwamba wasanii wengi nchini Kenya hawana kitu wanajibeba tu mitandaoni lakini katika maisha ya kawaida hawana kitu.

“Celebs hawana kitu, wanaishi rentals, gari ni ya loan na haina fuel ama amepewa lift tu,” Mathenge aliandika kwenye instastories zake siku chache zilizopita.

Tamko hili la Mathenge ni kama halikupokelewa vyema na KRG ambaye Jumatano amempasha kwa kusema kwamba pengine alikuwa anajisemea mwenyewe na si kwa niaba ya wqasanii kwani wasanii huku nje wanazidi kukipiga sana kutafuta pesa kwa udi na ambari.

“Yeyote amabaye alisema kwamba wasanii hawana kitu huenda alijizungumzia mwenyewe. Wewe ukikosa pesa usidhani kila mtu hana hiyo pesa. Kitu najua mimi ni kwamba watu wako bize sana kukimbizana na begi huku wengine wako bize kusambaza umbeya tu,” KRG alisawazisha bao lake Mathenge.