Nyumba ya marehemu Papa Wemba kuwa 'Hifadhi ya Rumba' DRC

Muhtasari

• Wizara ya Utamaduni na Sanaa ilishirikisha ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kuangazia ufunguzi huo.

• Ufunguzi huo unafanyika sambamba na kumbukumbu ya miaka 6 tangu kifo cha mwimbaji huyo.

• Alikuwa mmoja kati ya wanamuziki maarufu sana barani Afrika na kote duniani.

Marehemu Papa Wemba alikuwa mmoja wa mastaa wakubwa wa rumba
Marehemu Papa Wemba alikuwa mmoja wa mastaa wakubwa wa rumba
Image: GETTY IMAGES

Nyumba ya nyota wa muziki wa Soukous ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- marehemu Papa Wemba inatarajiwa kufunguliwa rasmi leo Jumapili 24 Aprili 2022.

Nyumba hiyo ilinunuliwa na serikali ya DRC na sasa itakuwa "Hifadhi ya Rumba".

Wizara ya Utamaduni na Sanaa ilishirikisha ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kuangazia ufunguzi huo.

Ufunguzi huo unafanyika sambamba na kumbukumbu ya miaka 6 tangu kifo cha mwimbaji huyo.

Papa Wemba ambaye jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, alianguka na kufa jukwaani akiwatumbuiza maelfu kwa maelfu ya mashabiki wake waliojitokeza katika tamasha la muziki mjini Abidjan Ivory Coast mnamo Aprili 24, 2016.

'Villa Vieux Bokul ilinunuliwa na serikali ya DRCkwa kima cha dola 750 za kimarekani.
'Villa Vieux Bokul ilinunuliwa na serikali ya DRCkwa kima cha dola 750 za kimarekani.
Image: BBC/ MBELECHI MSOSHI

Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.

Alikuwa maarufu katika micharazo ya muziki wa Soukous,

Alikuwa mmoja kati ya wanamuziki maarufu sana barani Afrika na kote duniani.

Image: BBC/ MBELECHI MSOSHI

Hatua ya DRC kufanya nyumba ya Papa Wemba kuwa Hifadhi ya Rhumba inakuja miezi michache baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kitamaduni kutambua Rumba ya Congo, na kipatia hadhi ya kulindwa na Unesco.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na nchi jirani ya Congo-Brazzaville zinamiliki ufalme wa zamani wa Kongo - ambapo mtindo huo wa muziki ulianzia kulingana na ombi la pamoja la mataifa hayo mawili.

Image: BBC/ MBELECHI MSOSHI

Neno "rumba" lenyewe linatokana na neno la Kikongo navel, "Nkumba".

Baada ya kupata hadhi hiyo Rhumba ya Congo iliungana na tamaduni zingine kama muziki wa reggae wa Jamaica na chakula cha wachuuzi wa Singapore zilizo katika orodha ya Unesco ya "Urithi wa kitamaduni usioonekana wa wanadamu"