Kila mara wakinitumia DM wananiomba pesa,'Huddah Monroe afichua tabia ya wanaume wanaomtumia jumbe

Muhtasari
  • Huddah Monroe afichua tabia ya wanaume wanaomtumia jumbe
Huddah Monroe
Image: Facebook

Mwanasosholaiti  Huddah Monroe anatamani angekuwa mwanamume hii ni baada ya kupata Pre-menstrual (PMS).

Huddah, ambaye alisafiri hadi Nairobi hivi majuzi anasema hangelazimika kukumbana na athari kama hizo za kabla ya kipindi kama angekuwa mwanamume.

Ikiwa kulikuwa na maisha ya pili, Huddah anasema anatarajia kuwa mwanamume kwa sababu ni rahisi sana.

ujauzito ni mbaya zaidi, wanaume wana kazi moja tu," aliandika kwenye chapisho la mtandao wa kijamii.

Huddah alifafanua kuwa anapenda kuwa mwanamke, lakini sio mambo ya ziada yanayoambatana nayo.

Huddah aliendelea kuwaita wanaume walio na wahusika wa kuchekesha, kama wale wanaofikiri wanaweza kuzima kiu yao kwenye DM zake.

"Nikimfuata mwanamume kwenye mitandao ya kijamiikinachofuata ni DM,LOL mnakiu ata DM na kuomba pesa," alisema.

Hivi majuzi, sosholaiti huyo alifunguka kuhusu aina ya wanaume anaowapenda.