Nitamshukuru Mungu kwa kunipa baba kama wewe-Rashid Abdalla amkumbuka marehemu baba yake

Muhtasari
  • Rashid Abdalla amkumbuka marehemu baba yake

Mwanahabari Rashid Abdalla anafahamika sana kupitia usemi wake wa 'sisemi kitu.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram  amesimulia jinsi inauma na ilivyouma baada ya kumpoteza maharemu baba yake.

Kulingana na mwanahabari huyo baba yake aliaga dunia mnamo mwaka wa 1996,ila anamshukuru Mungu kwa kumpa baba kama yeye.

Rashid alipakia picha ya kitambo ya baba yake na kuandika ujumbe wa kumtakia baba yake anedelee kupumzika kwa amani.

Kumpoteza baba yake kunaonekana kumwathiri Rashid kwani kila mwaka amekuwa akimkumbuka baba yake na kuwauliza mashabiki wamuombee.

"#sisemikitu Tarehe kama ya leo 1996 babangu uliye rafiki yangu uliaga dunia. Daima ntamshukuru Mungu kwa kunipa baba kama wewe. Endelea kulala pema Mr. Abdallah, Mwenyezi Mungu akulinde na adhabu ya kaburi, akusamehe dhambi zako za siri na dhahiri. Siku ya hesabu ukabidhiwe kitabu chako kwa mkono wa kulia Inshallah Amin," Aliandika.