Hakuna mtu anayepaswa kudharau msanii-DJ Shiti asema baada ya Khaligraph kusimulia haya

Muhtasari
  • Huku akisimulia wakati huo, Khaligraph alisimulia kisa kilichotokea mwaka wa 2012 kabla ya kufahamika sana
dj-shiti-2
dj-shiti-2

Wikendi iliyopita ilikuwa njema na ya kufana kwa rappa maarufu nchini Khaligraph Jones.

Hii ni baada ya kuwatumbuiza mashabiki wake Nyahururu  na kuheshimika sana.

Huku akisimulia wakati huo, Khaligraph alisimulia kisa kilichotokea mwaka wa 2012 kabla ya kufahamika sana.

Kulingana na msanii huyo alienda kuwatumbuiza mashabiki ilhali hakulipwa pesa zote ambapo anadai alidhulumiwa kama msanii.

"Mara ya 1 nilipoenda Nyahururu ilikuwa mwaka wa 2012, rafiki yangu aitwaye @romiswahili Alikuwa na uhusiano na Baadhi ya watu waliokuwa na hafla nilitakiwa kulipwa 7k lakini kwa sababu hakuna aliyejua mimi ni nani, waliishia kunipa 4k, ambayo pia ilitakiwa kuhudumia usafiri wa kwenda na kurudi, hapakuwa na mahali pa kulala.

Basi nililala kwenye Kituo cha mabasi nikisubiri basi la 1 lililokuwa likija Nairobi, Miaka 10 baadaye, mimi ni tajiri sasa, Mungu ni mwema, jana tuliua huko Nyahururu kwa mara nyingine tena na wakati huu OG aliheshimiwa," Khaligraph asimulia.

Mcheshi DJ Shiti akijibu ujumbe wake Khaligraps amedai kwamba hamna mtu ambaye anapaswa kumdharau msanii kwani siku hazifanani.

"Hakuna mtua anayestahili kumdharau msanii siku hazifanani kesho unaweza ukashangaa!!!!! 🔥🔥🔥🔥🔥🔥," Shiti Alisema.