Watu watanisherehekea na kufanya muziki wangu uvume nikifa-Avril

Muhtasari
  • Hata hivyo amekuwa kimya, na hii ni kwa miaka 4 iliyopita tangu alipojifungua mtoto wake wa kiume
Msanii Avril
Image: AVRIL/INSTAGRAM

Avril ni mmoja wa wasanii wa kike maarufu nchini,Amekuwa kwenye tasnia ya muziki kwa karibu miaka 20, na amekuwa akiacha nyimbozilizovuma na kupendwa na mshabiki kila mwaka.

Hata hivyo amekuwa kimya, na hii ni kwa miaka 4 iliyopita tangu alipojifungua mtoto wake wa kiume.

Akizungumza katika mahojiano na Mungai Eve, Avril alisema kuwa safari ya kuwa mama si mzaha lakini anafurahi kwamba ana mfumo mzima wa ikolojia karibu naye.

Msanii huyo  Alisema J Blessing na familia yake wamekuwa wakimuunga mkono na kila kitu kinachohusiana na uchumba na maisha ya uhusiano ni sawa.

Avril alisema kwa sasa anajishughulisha na mambo mengi ndiyo maana kila mwaka anaachia wimbo mmoja tu.

Uvumi ulienea mitandaoni kwamba Avril yuko single, lakini akiwa kwenye mahojiano hayao alisema kwamba yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi, na uhusiano ambao unapeneza.

Haya basi kwa wala ambao wamekuwa waiulizia yuko wapi msanii huyo amewajibu na kuweka wazi sababu ya kuachia kibao kimoja kila mwaka.