'Ulikuwa unatuma fare ama,'Rue Baby amuuliza shabiki aliyetapeliwa kwa jina lake

Muhtasari
  • Je ukija kanairo ushawahi tapeliwa kwa jina la mtu mashuhuri au msanii yeyote, kwani wengi wamejipata katika mtego huo
Rue Baby
Image: Hisani

Je ukija kanairo ushawahi tapeliwa kwa jina la mtu mashuhuri au msanii yeyote, kwani wengi wamejipata katika mtego huo.

Kuna baadhi ya watu ambao wamepoteza mamilioni ya pesa na hata wengi wao kupoteza biashara zao kutokana na ukora wa kutapeliwa.

Mwanawe msanii maarufu nchini Akothee,Rue Baby, amewatahadharisha mashabiki wake, baada ya mmoja wa mashabiki wake kutapeliwa elfu mbili.

Kulingana na Rue huwa hatumii picha zake kwenye ukurasa wake wa WhatsApp.

Mwanamitindo huyo aliweka wazi na kusema kwamba simu yangu huwa haichaji,huu akimjibu shabiki huyo alimuuliza iwapo alikuwa natuma pesa za nauli alipokuwa ana tapeliwa.

"Lakini ata wewe ukituma ilikua fare ama nini, watu wengi unifanya nicheke,tafadhali usitapeliwa, hata situmii picha yangu kweye whatsapp ," Rue Aliandika.