Raila ametusaidia kama wasanii-Msanii Ringtone adai

Muhtasari
  • Kulingana na Ringtone bendi hiyo inapaswa kumshukuru Raila Odinga kwa yale ametenda kupitia skiza Tune za vibao vyao
Image: INSTAGRAM// RINGTONE APOKO

HUku akizungumzia vita kati ya bendi ya muziki Sauti Sol na muungano wa kisiasa Azimio, zilizozuka mapema wiki hii msanii Rintone Akopo amedai kwamba kinara huyo wa ODM amewasaidia wasanii.

Kulingana na Ringtone bendi hiyo inapaswa kumshukuru Raila Odinga kwa yale ametenda kupitia skiza Tune za vibao vyao.

Bendi hiyo ilitishia kushtaki muungano wa Azimio kwa kutumia kibao chao wakati wa kumtambulisha Karua kama mgombea mwenza wa Raila katika uchaguzi mkuu ujao.

Huku chama cha ODM kikijibu madai hayo kilidai kwamba ilikuwa onyesho la upendo na mojawapo ya njia ya kushukuru bendi hiyo kwa kazi yai nzuri ambayo wanafanya katuka tasnia ya burudani.

Ni vita ambavyo vimeshuhudia bendi hiyo kupoteza zaidi ya  'subscribers' 2000, kwenye Youtube.

"Raila hata kama sio president ametupigania kuhusu mambo ya skiza tune. Tulikua tunapata 28% ya mapato lakini sasa tunapata 52%. Kwa mfano mimi nilikua napata Ksh 700k lakini saai napata Ksh 2.1 million monthly. Hiyo ni kama mshahara wangu sasa

Nyinyi mnajua sheria. DJ akitaka kucheza wimbo wako hatashida ameenda kwa kila msani kusign contract na wao," Alisema Ringtone kupitia kwenye video aliyopakia kwenye ukurasa wake wa instagram.