Nilikuwa na msongo wa mawazo-Flaqo afichua sababu ya kuchukua mapumziko kutoka kwa ucheshi

Muhtasari
  • Flaqo afichua sababu ya kuchukua mapumziko kutoka kwa ucheshi
Mchekeshaji Flaqo Raz
Mchekeshaji Flaqo Raz
Image: Instagram

Mchekeshaji maarufu mtandaoni Flaqo hatimaye amefichua sababu iliyomfanya kuchukua muda wa kutayarisha maudhui na kwa nini amekuwa kimya kwa mwaka 1 uliopita.

Akizungumza katika mahojiano , Flaqo alisema kuwa alilazimika kupumzika kwa sababu ya matatizo ya afya ya akili.

Alisema kuwa alikuwa maarufu akitengeneza pesa lakini hakuwa na furaha sana, na hakuna kitu kilichokuwa kikimsisimua.

Alisema alikuwa na aina fulani ya mshuko-moyo, na angeweza tu kujipata mpweke na kumwaga machozi.

"Nakumbuka nilimaliza shoot, nakwa na hisia fulani,Bien nakili haya, nilimpogia Bien simu nikaanza kusema mambo hata hayana maana,alinipa namba ya simu ya mtaalamu, ilikuwa hisia fulani sijui niseme Bipolar au Depression, nimekuwa nikipigana na hayo kwa mwaka mmoja sasa," Alieleza Flaqo.

Flaqo alisema imekuwa safari ngumu kwake kupata nafuu na kuwa kawaida.

Amekuwa akionana na mtaalamu kwa mwaka 1 uliopita na angalau sasa mambo ni sawa. Sasa anapanga kurejea tena katika tasnia ya uundaji wa maudhui, na yuko tayari kuzindua onyesho lake mwenyewe.

Sio Flaqo pekee ambaye amejitokeza na kusema kwamba alikuwa ama amekuwa akipambana na msongo wa mawazo bali tumewaona watu mashuhuri tofauti wakisema na kukiri kwamba msongo wa mawazo ni wa kweli.