Mwigizaji Nyce Wanjeri afichua jinsi alibaguliwa baada ya wazazi wake kuaga dunia

Muhtasari
  • Mwigizaji Nyce Wanjeri afichua jinsi alibaguliwa baaada ya wazazi wake kuaga dunia
Nyce Njeri
Nyce Njeri

Mwigizaji maarufu Nyce Wanjeri, anayejulikana zaidi kwa majina ya kisanii Shiru kwenye kipindi cha NTV Auntie Boss  amesimulia kwa hisia jinsi alivyokataliwa na familia yake.

Katika mahojiano na mwanahabari Monica Kagoni, Nyce alisema kuwa familia yake ilimbagua kila mara,Shangazi zake wangempa kaka yake chakula, zawadi na kumnyima.

Alijitahidi kadiri awezavyo kuwafaa kwa kuwasaidia na kazi za nyumbani.

Ilichukua muda kwake kutambua kwamba sababu iliyowafanya wambague ni kwa sababu mama yake alikuwa amempata kutoka katika uhusiano wa zamani kabla ya kuolewa na babake wa kambo ambaye kila mara ingawa alikuwa baba yake mzazi.

Mambo yalizidi kuwa mabaya zaidi mamake alipougua na kugundulika kuwa na VVU/UKIMWI.

Baba yake wa kambo pia alipatikana na ugonjwa huo. Alikufa baada ya muda mfupi lakini mama yake alipigana kwa miaka zaidi. Hakukuwa na ARV wakati huo.

Baada ya kifo cha baba yao, umaskini ulikuja. Nyce na kaka yake walitatizika kuongeza karo hadi wakafikiri kwamba wataacha shule lakini kwa msaada wa wasamaria wema walioingia baada ya kifo cha mama yao, walisoma wote hadi kidato cha nne.

Baada ya kidato cha nne, Nyce alibaini kuwa ana kipaji cha uigizaji.

Akiwa anaishi na binamu yake jijini Nairobi, alienda kwenye majaribio katika ukumbi wa michezo wa Kitaifa wa Kenya ambapo alipita na kupata nafasi ya kukuza talanta yake.