Zari Hassan atangaza kuzuru Kenya, Je kuna ni?

Muhtasari
  • Zari alikuwa nchini Kenya mnamo Mei 2018 kwa Tamasha la Colour Purple Concert lililofanyika katika bustani ya Uhuru Gardens Nairobi
Zari Hassan
Image: Maktaba

Mfanyibiashara  Zari Hassan ametangaza kuzuru Kenya wiki hii.

Zari kupitia mtandao wake wa kijamii alisema kuwa atahudhuria karamu  katika klabu ya XS Millionaires siku ya Alhamisi.

Zari aliwaomba mashabiki wake wa Kenya wajiunge naye wanaposhiriki sherehe pamoja.

"Wacheza mpira wote jijini Nairobi wajitayarishe kwa tajriba ya weupe katika klabu ya XS Millionaires jijini Nairobi Alhamisi hii Juni 9. Nitahudhuria pamoja na wapiga mipira wengine, come lets pop champagne pamoja. Tuonane Alhamisi katika klabu ya mamilionea ya XS."

Zari a aliongeza kuwa alifurahia safari yake nchini Kenya.

"Ninatazamia kufichua muundo mkubwa wa jumba kubwa. Nimefurahishwa na safari yangu ijayo ya Nairobi hivi karibuni! Ungana nami na @fine_urban_co_interiors_ltd tunapofichua jumba la kifahari. Ninapenda kazi yao nzuri na siwezi kungoja kuwa huko nijionee mwenyewe. Hutaki kukosa hii!"

Zari alikuwa nchini Kenya mnamo Mei 2018 kwa Tamasha la Colour Purple Concert lililofanyika katika bustani ya Uhuru Gardens Nairobi.

Hafla hiyo ilikuwa ni ya uwezeshaji wa wanawake na ufahamu wa saratani.