Mcheshi wa Churchill Show Nasra na mumewe watarajia mtoto wao wa kwanza

Muhtasari
  • Habari hizo kubwa zilifichuliwa na wanandoa hao  kupitia post zao kwenye akaunti zao za Instagram

Wacheshi maarufu wa Kipindi cha Churchill Nasra Yusuf na Rashid Abdalla wanatarajia mtoto wao wa kwanza pamoja.

Habari hizo kubwa zilifichuliwa na wanandoa hao  kupitia post zao kwenye akaunti zao za Instagram, ambapo waliweka picha wakiwa pamoja wakionyesha matokeo ya kipimo cha ujauzito.

Akiwa na furaha tele, Nasra Yusuf aliandamana na picha hiyo na nukuu inayotiririsha tukio hilo muhimu.

"Hii ndiyo furaha ambayo nimekuwa nayo kwa muda mrefu. Nina penzi la mwanamke ambaye bado sijakutana naye...siwezi kusubiri kukutana nawe mtoto wangu...fikiria kuwa na mtoto mwenye penzi la maisha yako. Nakupenda @director_rashid" aliandika.

Kwa kutumia akaunti yake ya Instagram, Rashid pia aliandika;

"Nimekuwa nikisubiria haya yatokee kwa muda na hatimaye Mwenyezi Mungu amefanikisha alhamdulillah. Siwezi kusubiri kukutana na wewe mtoto wangu. Utakuwa mzuri kama mama yako @na