'Nakupeza kila siku,'Mkewe Nyashinski amsherehekea marehemu dada yake

Muhtasari
  • Mkewe Nyashinski amsherehekea marehemu dada yake

Mfanyibiashara na mkewe rapa Nyashinski Zipporah Jepkemei maarufu Zia Bett ameandika ujumbe mzuri kwa dadake marehemu Janet Bett aliyefariki Oktoba 2021.

Katika ujumbe mzito wa siku yake ya kuzaliwa, Zia alimweleza dada yake jinsi maisha yalivyokuwa tangu aondoke, huku akikiri jinsi anavyomkumbuka haswa katika siku yake ya kuzaliwa.

Mwanzilishi wa Zia Africa pia alisherehekea marehemu dadake kama rafiki yake wa karibu na bora ambaye angeweza kukaa muda mrefu zaidi duniani.

"Heri ya kuzaliwa ukiwa mbinguni Janet Bett! 🎈Najua Mbinguni ilihitaji malaika zaidi, ndio maana walikuita huko. Natamani wangechelewe kwa muda mrefu zaidi. Ninakukumbuka kila siku, lakini haswa leo. Najua tutakutana tena katika Umilele. Nakupenda sana. Heri ya siku ya kuzaliwa, dada yangu mpendwa na rafiki bora,” unasoma ujumbe wa Zia kwa marehemu dadake.

Janet Bett aliaga dunia baada ya kuugua ugonjwa wa Severe Aplastic Anaemia, mnamo Oktoba 2021, hali ambayo alikuwa amepambana nayo kwa muda.