Sitawahi mtambulisha mpenzi au mke wangu mitandaoni-Mwigizaji Govi akiri

Muhtasari
  • Ana imani kubwa kwamba uhusiano lazima uhifadhiwe faragha
  • Aliendelea na kusema kwamba hata gari lake hatalionyesha mtandaoni, anataka tu maisha yake ya kibinafsi yawe ya faragha sana
Image: INSTAGRAM// MALIK LEMMY

Shinikizo limekuwa kali mitandaoni hasa kwa watu maarufu,waigizaji,wasanii,waunda maudhui, huku wengi wakianika maisha yao mitandaoni.

Lakini je sababu ya wengi kuanika maisha yao mitandaoni na kukabiliana na changamoto za mitandaoni ni ipi?

Aliyekuwa mwigizaji wa kipindi cha Machachari Malik Lemmy maarufu kama Govi ​​amezua tafrani tena mtandaoni baada ya kufichua hadharani kuwa hatawahi kumtambulisha mtu anayechumbiana naye mtandaoni au hata siku zijazo mtu ambaye atafunga naye ndoa.

Govi alisema kuwa mitandao ya kijamii ina shinikizo na chuki nyingi.

Hataki mtu yeyote ampendaye apitie yale ambayo yeye binafsi amepitia kwa hiyo jambo bora zaidi ni kuweka uhusiano wake kuwa wa faragha na kuzingatia tu uigizaji na kile kilichompa umaarufu.

Aliendelea na kusema kwamba hata gari lake hatalionyesha mtandaoni, anataka tu maisha yake ya kibinafsi yawe ya faragha sana.

Tofauti na rafiki na kaka yake mkubwa katika uigizaji Tyler Mbaya ambaye anafanya maudhui ya wanandoa, Govi ​​alisema kuwa kwake hilo haliwezi kutokea na kamwe halitatokea.

Ana imani kubwa kwamba uhusiano lazima uhifadhiwe faragha.

"Mitandao ya kijamii ina shinikizo mini sana, watu walinifahamu kupitia uigizaji kwa hivyo wacha wanitambue kwa hilo na wal sio kuanika maisha yangu mitandaoni."