Mbarikiwe,'Akuku Danger na Sandra Dacha wawashukuru Wakenya kwa kufanya haya

Muhtasari
  • Jumatano, Akuku alisema kulazwa hospitalini mara nyingi mwaka huu kumemdhoofisha kiakili, kifedha na kimwili
Sandra Dacha almaarufu kama Silprosa na mpenzi wake Akuku Danger
Sandra Dacha almaarufu kama Silprosa na mpenzi wake Akuku Danger
Image: INSTAGRAM// SANDRA DACHA

Chini ya saa 24, Wakenya na mashabiki wa mcheshi Akuku Danger wameonyesha upendo wao kwa mcheshi huyo baada ya kuchanga zaidi ya nusu milioni.

Hii ni baada ya mcheshi huyo kutoa wito kwa wakenya wamchangie baada ya kuzuiliwa hospitali kwa kutolipa bili ya Sh883,000.

Akuku amekuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi West baada ya kulazwa takriban wiki mbili zilizopita.

Jumatano, Akuku alisema kulazwa hospitalini mara nyingi mwaka huu kumemdhoofisha kiakili, kifedha na kimwili.

Ameeleza kwamba ugonjwa wa Sickle Cell Anemia ambao alizaliwa nao ndio umekuwa ukimwathiri kiasi cha kulazwa.

"Imekuwa changamoto lakini bado ninashikilia. Msichoke na Mimi," Akuku aliwaomba Wakenya.

Kupitia kwenye ukurasa wa Sandra wa instaram amefichua kwamba wakenya wamechanga zaidi ya elfu mia tano, kwa saa 20,huku akiwashukuru kwa kitendo hicho.

"Elfu mia tano kwa saa 20,aki wakenya nyinyi nitasema nini," Alisema Sandra Dacha.

Akuku Danger naye alisema;

"Mbarikiwe."