"Siwezi sema kwenye wimbo kilichotokea baina yangu na Arnelisa" - Ben Pol

Muhtasari

• "Tutaimba muziki tutacheza party nini vitu kama hivyo kwenye jumbe lakini si kuimba hadithi ya maisha yangu kwenye wimbo" - Ben Pol

Msanii Ben Pol kwakati wa mahojiano
Image: Mpasho (YouTube screenshot)

Msanii kutokea Tanzania Ben Pol ameweka wazi jinsi alivyohisi baada ya Arnelisa Muigai kumtema na kuivunja ndoa yao ambayo walikuwa wameifunga katika kanisa ya kikatoliki, jambo lililomfanya mwanamuziki huyo mpaka kubadili dini kwenda Uislamu.

Akizungumza na Mpasho wakati wa ziara yake nchini Kenya kuitangaza mradi kwa jina la Kijanisha, mradi unaohubiri umuhimu wa kufanya mazingira kuwa kijani. Kijanisha vilevile ni jina la wimbo ambao sanii huyo ameshirikiana na wasanii wenzake kina Christine Shusho, Joh Makini na Fridah Amani kama njia moja ya kutangaza mazingira kijani kote Afrika, Ben Pol alisema kwamba kuvunjika kwa ndoa yake na Arnelisa Muigai lilikuwa ni jambo ambalo lilimvunja moyo sana mpaka kufikia hatua ya kutojielewa kabisa.

“Baada ya chochote kilichotokea kwenye maisha yangu binafsi naamini kama uliwekezwa kama nilivyokuwa huwezi kutoka na kuendelea kama kawaida hivyo ilinibidi kustahimili na kwa utaratibu wa kukabiliana na hali nilienda kwa ushauri siwezi kukanusha,” alisema Ben Pol.

Kuachia mbali Sakata hilo a kuachana kwao muda mfupi tu baada ya kufunga ndoa ya kikatoliki, mwanamuziki huyo alifichua kwamba hakuendelea kuweka uadui na aliyekuwa mke wake Arnelisa bali huwa wanazungumza na anamtakia kila la kheri katika maisha.

Mwanamuziki huyo alisema kwamba katu hajutii kile ambacho kiliikuta ndoac yake na Arnelisa na kusema kwamba alishakubali kwamba yalimwagika na kamwe kuzoleka ni mwiko kwa hiyo ni kuchukua mafunzo tu.

“Nikiskia niko ready I would get married sitafuti mtu lakini ikitokea I am free-spirited unajua I am just living my life genuinely the universe itaniletea watu whether ni friend or partner itani letea the right people kwa mda ambayo ita fanya, siwezi sema natafuta sitafuti mimi. Ninafurahia watu,” Ben Pol aliiambia Mpasho.

Alipoulizwa kama yupo tayari siku moja kutoa wimbo ama kuandika kitabu kuelezea mashabiki wake kile kilichosababisha kuvunjika kwa ndoa yake na mrithi huyo wa kampuni ya kutengeneza mivinyo ya Keroche, Ben Pol aliguna kiasi na kusema kwamba hana uhakika wa kufanya jambo kama hilo kwani chochote kilichotokea ni baina yao wawili.

“Sidhani kama nitafanya hivo kwa sababu, yaani mimi naona haitapendeza kwa sababu mimi sidhani kwamba kukuwa artist ndio kila kitu chako kiwe nje tena, nadhani hiyo ni maisha ya kibinafsi na sidhani litakuja jambo zuri. Tutaimba muziki tutacheza party nini vitu kama hivyo kwenye jumbe… labda kama ni kwa njia ya kumotisha ninaweza fanya lakini si kwa njia ya kusema hadithi yangu mimi kwenye wimbo, hiyo mimi sitaweza” alijibu Ben Pol.