"Alimtambulisha kwangu kama rafiki yake" Ib Kabba azungumzia mpenzi mpya wa Amber Ray

Ib Kabba alilalamika kwamba huenda Amber Ray walikuwa wanamzunguka kimapenzi na mpenzi wake mpya kwa sababu alimtambulisha mwanzoni kama rafiki tu

Muhtasari

• Inaonesha wazi kwamba nyinyi watu mlikuwa mnafanya mambo yenu ya kisiri hata wakati tulikuwa tunachumbiana

Ib Kabba na Amber Ray kipindi wakiwa wapenzi
Image: Maktaba

Aliyekuwa mpenzi wa mwanasosholaiti Amber Ray, Ib Kabba, mwanaume kutoka taifa la Sierra Leone ametoa maoni yake kuhusu suala lililosambaa mitandaoni la mwanamitindo huyo kumtambulisha mpenzi wake mpya baada ya wawili hao kubwagana wiki kadhaa zilizopita.

Mwanamitindo Amber Ray Jumatano alipakia picha kwenye Instagram yake akiwa na mwanaume ambaye katika maelezo alifuatisha nayo picha ile ya pamoja iliashiria wazi kwamba ni mpenzi wake mpya.

“AMBAYE unapitia maisha naye katika wakati huu ni mbaya zaidi sasa kuliko hapo awali. Kwa mengi yanayotokea karibu na moja kwa moja kwetu, chagua upendo wako, marafiki zako, nafasi zako salama kutoka kwa wale ambao wanaweza kukupa huruma na kugusa unavyostahili na kuhitaji. #MyG,” aliandika Amber Ray.

Baadae mpenzi wake wa zamani kutoka Sierra Leone, Ib Kabba aliandika kwenye instastories zakeakielezea kwamba ni kweli anamjua mwanaume huyo na kusema kwamba hashtuki Amber Ray kumtambulisha kama mpenzi wake mpya kwani alikuwa anamjua na walikuwa marafiki wa kufanya mambo mengi pamoja.

Kabba alielezea kwamba Ray mwenyewe ndiye alimutambulisha mwanaume huyo kwake kama Rafiki na wakawa wanafanya mambo mengi pamoja ila jambo la yeye sasa kutambulishwa kama mpenzi ni suala jingine linalochukua mkondo tofauti kabisa.

“Inachekesha sana kwa sababu baada ya kumtambulisha mwanaume kwangu kama Rafiki, mpaka tukawa tunakula pamoja mara ghafla naona mwanaume huyo huyo anatambulishwa tena kama mpenzi kwa kweli inaonesha wazi kwamba nyinyi watu mlikuwa mnafanya mambo yenu ya kisiri hata wakati tulikuwa tunachumbiana. Ni ukichaa mkubwa sana, ogopa wanawake,” aliandika Ib Kabba.

Hivi majuzi Amber Ray alizuka kwenye gumza la mitandaoni tena pale aliposema kwamba yupo tayari kutulia kwenye ndoa pindi atakapoipata kwa sababu maisha yamekuwa magumu na uchumi kuporomoka kwa maana hiyo alikuwa tayari kutulia kwenye mahusiano ili kupata usaidizi kimaisha.

Mwanamitindo huyo ambaye haishi vituko alikuwa mpenzi wa mfanyibiashara wa matatu Jimal Rohosafi ambapo ilisemekana kuwa aliolewa na mfanyibiashara huyo kama mke wa pili, ila mahusiano yao yalivurugika miezi michache baadae kutokana na purukushani na mke wa kwanza wa Jimal, Amira.

Ray alichukuwa hatua ya kuonesha kwamba amemalizana na mahusiano yake na Jimal pale alipopakia video akiifuta tattoo ya mfanyibiashara huyo ambaye alikuwa ameichora mwilini mwake kama ishara ya mapenzi.