DJ Pierra Makena alazimika kukatiza safari ya Marekani baada ya bintiye kulazwa hospitalini

Muhtasari
  • Mama huyo wa mtoto mmoja aliwaomba radhi mashabiki wake wa Marekani, akieleza kwamba inabidi ahakikishe binti yake yuko vizuri kabla ya kuondoka nchini

Mcheza santuri  wa Kenya Pierra Makena amelazimika kukatiza ziara yake nchini Marekani ili kumuuguza bintiye Ricca Pokot ambaye kwa sasa amelazwa hospitalini.

Mama huyo wa mtoto mmoja aliwaomba radhi mashabiki wake wa Marekani, akieleza kwamba inabidi ahakikishe binti yake yuko vizuri kabla ya kuondoka nchini.

Hata hivyo, aliahidi kufanya hivyo kwa mashabiki wake wa marekani  baadaye.

“Nilitakiwa kuwa kwenye ndege leo kuelekea Marekani. Lakini mimi hapa. Mtoto wangu amekuwa mgonjwa na amekuwa mbaya zaidi. Ilinibidi kughairi safari ili tu nimtunze na kuwa naye.

"MN na Dallas naomba ufahamu na maombi yenu na miji mingine yote baada ya wikendi hii kwa huruma ... lakini tutafanya hivi tena ... nitashiriki tarehe mpya. Nawapenda ninyi nyote na mwombee Ricca,”Aliandika Pierra.

Mashabiki na wanamitandao walimtumia mwanawe Pierra jumbe za afueni ya haraka na za kumtia nguvu