Grace Mwai,fena Gitu waachia kibao kipya cha Martha Karua

Muhtasari
  • Heko Mama ni wimbo wa kampeni wa Martha Karua na Raila Odinga, unaoangazia nguvu za mama
Martha Karua
Image: MARTHA KARUA/TWITTER

Mgombea mwenza wa urais wa muungano wa Azimio la Umoja Martha Karua ameshirikishwa katika wimbo mpya unaoitwa Heko Mama.

Wimbo huu unaweka pamoja juhudi za pamoja za wasanii Fena Gitu, Sally Wisdom, Grace Mwai na Jecinta Omondi.

Mcheshi Joe Nyokabi, ambaye alivuma sana baada ya kuiga hotuba ya Martha Karua kwenye video ya kufurahisha pia aliangaziwa kwenye wimbo huo.

Heko Mama ni wimbo wa kampeni wa Martha Karua na Raila Odinga, unaoangazia nguvu za mama.

Wimbo huo unalinganisha Kenya na mama.

Katika wimbo huo wanamlinganisha Martha Karua huku mama wa taifa akimsihi kusimama kidete akisema ni wakati wake kuwaokoa wakenya jinsi mama anavyopaswa kufanya.

Wanamwambia asichoke kwa sababu ameshindwa mara nyingi na kudharauliwa lakini ni wakati wake wa kusimama tena na kulibeba taifa mgongoni kwenye mafanikio.

Martha Karua loves music and last week she joined Sally, Grace, Jecinta, and Fena for the recording of the Heko Mama music video. She made sure Harooo man joined her. This is a song that celebrates how far Mama Kenya has come. #Inawezekana #NikoSureNaBaba #NikoSureNaMartha