Ben Pol - Niliwahi iba daftari nikiwa shule, kipindi cha furaha zaidi ni wakati mwanangu alizaliwa

Ben Pol alisema angependa kuadimika muda anopatikana lakini pia akasema jambo hilo litamuuliza sababu amezoea kujumuika na watu.

Muhtasari

• ""Tuliwahi iba kitabu na rafiki yangu kipindi tunasoma lakini si jambo ambalo najivunia" - Ben Pol

msanii Arnelisa Muigai
Ben Pol msanii Arnelisa Muigai
Image: Instagram

Msanii wa bongo fleva Ben Pol ambaye yupo nchini kwa hafla moja ya kuhubiri umuhimu wa kuyafanya mazingira kuwa kijani amefunguka mambo ya ndani kuhusu maisha yake, vitu ambavyo mashabiki wake wengi hawavijui kumhusu.

Katika kipindi kimoja cha kujibu maswali ya haraka almaarufu ‘Quickfire’ na kituo kimoja cha redio nchini, Ben Pol alifunguka ukweli wa maisha yake kwamba aliwahi iba kipondi yupo shuleni.

Msanii huyo alisema aliiba daftari kwa ushirikiano na Rafiki yake, kitabu ambacho walikitumia kutunga mashairi ya nyimbo.

“Umewahi iba kitu chochote?”

“Nafikiri ndio, wakati nasoma shule, mimi na Rafiki yangu tuliiba daftari tukawa tunaandika mashairi, tunacheza beats kwenye tape, na si kitu amabacho ninajivunia ila ukweli ni kwamba niliiba,” msanii huyo alijibu.

Aipoulizwa kuhusu wakati wa furaha zaidi katika maisha yake, wengi walidhani angesema ni kipindi alifunga pingu za maisha na aliyekuwa mpenzi wake, mrithi wa kampuni ya kutengeneza mvinyo ya Keroche, Arnelisa Muigai. Lakini si kweli.

Ben Pol alisema kwamba wakati unaokwenda kwenye kumbukumbu zake kuwa wenye furaha zaidi maishani mwake ni wakati mtoto wake wa kiume alizaliwa. Awali msanii huyo alifichua kwamba kabla ya ujio wa Arnelisa katika maisha yake, alikuwa katika mahusiano ambapo alifanikiwa na mtoto wa kiume ambaye kwa sasa ana miaka sita.

Pia kitu kingine ambacho alishangaza wengi ni wakati aliulizwa kitu ambacho anaweza kukibadilisha katika maisha yake naye akasema kwamba labda akipewa nafasi atataka kuadimika sana ila pia akasema hilo litamuuliza kwa kuwa amezoea kujumuika na watu.

“Ningependa kubadilisha kupatikana kwangu, sitaki kupatikana kwa sababu muda mwingine nachoka sana. Kwa mfano unaezapata watu mia wanataka kupiga picha na unachoka kinoma lakini huwezi sema hapana, mambo kama hayo,” Ben Pol alisema.

Msanii huyo waliachana na aliyekuwa mke wake halali wa ndoa takatifu Arnelisa Muigai mwaka jana, miezi michache tu baada ya kufunga ndoa iliyohudhuriwa na umati wa waumini wa kanisa katoliki, jambo lililompelekea kusemekana kuwa amebadilisha dini na kuwa Muislamu.