"Wanadada wanaota wakiwa katika ndoa na mimi, wananitafuta kuniambia" - Mbosso

Mbosso alieleza kwamba mwanamke mmoja alimfuata kutoka Tabora kumwambia ameota kufanya ndoa na yeye.

Muhtasari

• Mbosso alielezea kwamba wanawake wengi wanamfuata na kumwambia wanamuombea na kuoteshwa ndoa na yeye.

Msanii Mbosso katika mahojiano ya refresh
Mbosso Msanii Mbosso katika mahojiano ya refresh
Image: Wasafi Media (Youtube screengrab)

Msanii wa WCB, Mbosso amefunguka ya moyoni  na ambayo yanastaajabisha mno ambapo anasema wanawake wengi tu wanamfuata wakimuambia kwamba wamejiwa na ndoto za kutaka kuoana na yeye.

Akizungumza kupitia kipindi cha Refresh cha Wasafi FM, Mbosso alitolea mfano kwamba kuna mwanadada mmoja kutoka eneo la Tabora nchini huo ambaye aliwahi mfuata na kumwambia mambo na ndoto.

“Hapa kwangu juzi amekuja dada ametoka Tabora amekaa kama siku tatu nje. Alisema yeye ameoteshwa alikuwa ameenda kusuali alivyotoka kumuombea Mbosso ndio akaokota hela na kuchukua basi kutoka Tabora kuja kwangu ili nimuoe,” alielezea Mbosso.

Msanii huyo alisemac kwamba kwa maelezo ya dada huyo baada ya kufanya maombi kwa ajili ya Mbosso, ghafla aliokota hela na hela hiyo hiyo akaifanya nauli ili kumfuata Mbosso akiamini kwamba kumuombea kulileta baraka ya kuokota hela kwa hiyo hakuona hatari ya kumfuata ili kumuomba ndoa.

Msanii huyo alieleza kwamba hiyo si mara ya kwanza kwani kuna mwanadada mwingine aliwahi kumfuata baada ya kumaliza kuhiji kwamba ameambiwa yeye ndiye mwanaume anayefaa kumuoa.

Mbosso alisemac amekutana na visa kama hivyo vingi sana.

“Nakumbuka pia kuna kipindi nilikuwa hapa kwetu gym nilikuwa nimeenda mazoezini akaja dada mmoja akanitoa ndoa akaniambia samahani kaka mamangu anakupenda sana halafu yupo kwenye gari naomba uje kumsalimia, anakupenda, anasali anakuombea sana yaani,” alikumbuka Mbosso.

Mbosso alishangaa tukio hilo ila ikabidi ameandamana na yule dada kwa ajili ya kumsalimia mamake kwenye gari na kweli alikutana na mama mtu akamsalimia na mpaka kumtilia dua.

Mbosso anafunguka kuhusu madai haya ya kina dada kuoteshwa kufanya ndoa naye kipindi ambapo msanii huyo mwenyewe kwa mara kadhaa amenukuliwa akisema kwamba huenda hatotaka kupata watoto kabisa au hata kuwa na mke katika maisha yake.