"Wakenya acheni ushamba, kubali mabadiliko!" Mwanafasheni atetea vazi la Nadia Mukami

Mwanafasheni wa msanii Nadia Mukami ametetea vazi alilotoka nalo katika tamasha lake mjini Meru.

Muhtasari

• “Nadia Mukami si Jirani yako useme utampangia jinsi ya kuvaa ili aonekane mama wa Kiafrika." mwanafasheni huyo alitema moto.

Nadia Mukami na mwanafasheni wake
Gold Melina, Nadia Mukami Nadia Mukami na mwanafasheni wake
Image: Instagram (Screenshots)

Mwanafasheni anayehakikisha muonekano wa mwanamuziki malkia wa humu nchini Nadia Mukami sasa amejitokeza wazi na kulitetea vazi alilotoka nalo kwenye video fupi msanii huyo kwenye Instagram yake.

Watu wengi baada ya kuiona nguo hiyo aliyotoka nayo Nadia walimkashfu vibaya wakisema kwenye fasheni kwa mara ya kwanza alifeli vibayaa.

Gold Melina, anavyofaamika mwanafasheni huyo aliamua kutolifumbia hilo macho na kupeleka maskitiko yake kwenye Instastory yake huku akiwakemea watu wanaoukosoa mtindo huo mpya wa Nadia.

Kulingana na nyingi za jumbe zilizoachiwa kwenye video hiyo, wengi walihisi Nadia ameenda sana na wala mambo kama hayo hayamkai sawa, wengine wakisema ni mitindo ya wasanii wa kike kutoka nchi za wazungu kule kina Beyonce.

“Please hapa hakuna cha haters or ushamba.. Tusidanganye warembo.. Hii ilikataa kabisa.. Na huo ndio ukweli wa maneno.. There is nothing like sijui body shamming.. Hapana kabisa.. Kitu mbaya ni mbaya... Hiyo fashion yangu haileti. shangwe..” aliandika shabiki mmoja ambaye pia ni polisi aliyepambwa sana kwa sifa, Sammy Ondimu Ngare.

Kwa maneno yake Melina, watu wengi wanaonekana kutoelewa maana ya fasheni na kuwataka wakome kuingilia jinsi anavyotaka kuvaa kwani si Jirani wao.

“Nadia Mukami si Jirani yako useme utampangia jinsi ya kuvaa ili aonekane mama wa Kiafrika. Kumbuka yeye ni mwanamuziki, mpeni nafasi ya kutalii fasheni. Wakenya wanataka kufikia ngazi za majukwaa ya kimataifa katika Sanaa, fungua bongo zenu na mkumbatie mabadiliko,” mwanafasheni Melina alifoka katika ujumbe mrefu alioupakia kwenye instastory yake.

Gold Melina pia aliwaosoa vikali wale waliokuwa wakiukosoa mtindo wa kutembea wa Nadia kwenye video hiyo na kusema kwamba hiyo moja kwa moja ni kumkosea heshima, pengine kwa kutojua changamoto ya kuzaa na kuwaita watu hao kuwa ni waoga wasiokuwa na hisia.

Akirudia nyundo yake kwenye msumari ule ule, Melina alisema kando na mambo yote bado Wakenya wanahitaji kukumbatia fasheni na kukubali mitindo mipya.

“Lakini tukija na maswala ya fasheni, watu inabidi wakumbatie fasheni nchini Kenya na wala sio kutaka kuziona huko kwa kina Beyonce. Nadia ni Beyonce wetu wa Kenya, sasa mbona aivalie kama yeye? Wakenya waache ushamba na kukomaa,” alimaliza kwa hasira Melina.