(Video) "Msinione kama mshindani, nikaribishe tufanye kazi pamoja" Ringtone awaambia wasanii wa kidunia

Ringtone aliwashukuru wasanii wote wa injili kwa kuwa na yeye kipindi amekuwa mwenyekiti wao.

Muhtasari

• “Nataka kuchukua hii fursa kuwashukuru wale wote ambao wamekuwa wakinisapoti kwenye Sanaa ya injili, ambayo sasa imefika mwisho." - Ringtone.

Msanii Ringtone Alex Apoko ambaye alijipadisha cheo na kujiita mwenyekiti wa wasanii wa injili nchini Kenya amewataka wasanii wanaoimba nyimbo za kidunia kumkaribisha na wasimuone kama ameleta ushindani katika upande huo wa Sanaa ya muziki.

Katika video ambayo aliipakia Jumanne alasiri, Ringtone amewataka wasanii wa miziki ya kizazi kipya kutomchukulia vibaya anapojiandaa kuanza kuimba miziki ya dunia nqa badala yake washirikiane kufanay kazi ya muziki wa kidunia pamoja.

“Wale wasanii ambao mnaimba nyimbo za mapenzi, naomba msinione kama mshindani wala msihisi kutishiwa. Tufanye kazi pamoja ndio tuweze kufikisha muziki mahali inafaa kufika. Kwaheri injili,” alisema Ringtone kwenye video aliyoipakia Instagram yake.

Awali, Ringtone alikuwa ametangaza kwamba ni rasmi safari yake ya kuimba miziki ya injili imefikia kikomo na kwamba ataanza kutunga mashairi ya kidunia.

Ringtone aliwashukuru wasanii wenzake katika kitengo cha injili kwa kumshikilia mkono muda huu wote amekuwa kama mwenyekiti wao na kusema sasa umefika wakati wa kuufungua ukurasa mpya wa maisha yake ya kimuziki.

“Nataka kuchukua hii fursa kuwashukuru wale wote ambao wamekuwa wakinisapoti kwenye Sanaa ya injili, ambayo sasa imefika mwisho. Wasanii kama kina Moji Shortbabaa, kina Guardina Angel na wengine, nataka kuwaambia ahsante kwa ile sapoti mmenipatia wakati nimekuwa mwenyekiti wenu, na sasa hivi nimetoka, mbarikiwe!” alimaliza Ringtone.

Ringtone ni miongoni mwa wasanii wakongwe kabisa na ambao wamekuwa bado wanapiga hatua za kimadhubuti katika injili ya kizazi kipya ambapo wenzake kama kina Bahati na Willy Paul walishagura kitengo hicho na kuanza kuimba miziki ya kidunia.

Ringtone amekuwa akiwakashfu pakubwa katika siku za nyuma huku akisema walimsaliti Mungu kwa kuacha kuimba injili na kuingilia miziki ya kidunia ambayo alisema huwa hasikizi lakini sasa inaonekana pia yeye anafuata mkondo huo huo, kama kile alichokisema kwenye video hiyo ni ukweli wa kusadikika.