(+Picha) “Ahsante Mungu kwa zawadi hii,” Hatimaye Nandy aweka wazi picha za ujauzito wake

Nandy na Billnass walivishana pete za uchumba mwezi Februari.

Muhtasari

• Wawili hao wanatarajia mwanao hivi karibu huku pia arusi yao ikitarajiwa kufanyika mwezi huu.

Wasanii ambao pia ni Wachumba Nandy na Billnass
Wasanii ambao pia ni Wachumba Nandy na Billnass
Image: Nandy (Facebook)

Baada ya ficha ficha za muda mrefu, hatimaye mwanamuziki Nandy ameweka wazi kwamba yeye na mumewe mwanamuziki na mjasiriamali Billnass wanatarajia zawadi ya mtoto hivi karibuni.

Kupitia kwa ukurasa wake wa Instagram, malkia huyo wa muziki wa bongo fleva alipakia picha inayomuonesha kabisa akiwa mjamzito pamoja na mumewe kando yake akiwa amechora ishara ya pendo kupitia vidole vyake vya mikono.

“Ahsante Mungu kwa zawadi hii,” aliandika Nandy.

Mastaa mbali mbali walifurika kwenye ukurasa huo na kuachia jumbe zao za kheri njema kwa familia hiyo changa huku wakiwapongeza kwa hatua hiyo kubwa ya kusubiria mtoto, kwani siku hizi ni wengi wanaowatafuta wana bila mafanikio.

Nandy amekuwa akisemekana kuwa mjamzito lakini kwa siku za hivi nyuma alikuwa anaficha na hata kukanusha madai hayo baada ya wambea wa mitandaoni kukisia kwamba kimya chake cha muda mrefu huenda kimesababishwa na malezi ya mimba.

Wiki hii muigizaji Steve Nyerere alikuja na jipya ambapo alisema kwamab wachumba hao wamempa mkataba wa kuhakikisha kuwa ndoa yao inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni inakwenda mbele kwa usawa wa kipekee kwa kumtaka awe mwenyekiti wa shughuli hiyo yenye kuandikisha kumbukumbu katika historia ya maisha yao.

Nandy na Billnass walivishana pete za uchumba mwezi wa pili mwaka huu ambapo Nenga, kama anavyofahamika Billnass na mashabiki wake alienda nyumbani kwao Nandy kule Mladizi na kumvisha pete ya uchumba kabla ya kulipa mahari.

Waliahidi kuwa harusi itafanyika miezi sita ijayo, na kusema kweli huu ukiwa ndio mwezi wa sita tangu uchumba, ni kweli minong’ono ya harusi imesikika na bila shaka hawataangusha jamii ya wanamitandao ambao wameisubiri ndoa hiyo sana.

Steve Nyerere ameipamba harusi hiyo mpaka kusema kwamba itakuwa ya kipekee kwa jina ‘wedding’ ambayo haijawahi kutokea katika ardhi ya Tanzania tangu uhuru miaka ya sitini.

Nyerere alisema wataomba mamlaka haki za kuiandaa harusi hiyo na kuitaka siku yenyewe itangazwe kuwa sikukuu ili wananchi wote wapate kushiriki kwa kuifuatilia moja kwa moja katika runinga.