"Sikuvunja ndoa ya Rayvanny na Faymah, ilikuwa kazi tu," - Video Vixen wa ngoma ya 'I Love You'

Nana ni video vixen ambaye amefanya kazi na wasanii wengi tu kutoka lebo ya Wasafi

Muhtasari

• Alisema yupo kwenye mahusiano na hata Rayvanny mwenyewe anajua mpenzi wake kwa hiyo hangeweza kufanya kitu cha kipuuzi.

Video Vixen maarufu nchini Tanzania, Nana
Video Vixen maarufu nchini Tanzania, Nana
Image: YouTube (Screengrab)

Video vixen Nana, mwenye alipamba katika wimbo wa msanii Rayvanny wa ‘I Love You’ hatimaye amefunguka makubwa na kuzungumzia minong’ono ambayo imekuwa ikienezwa mitandaoni kwamba ndiye alisambaratisha mahusiano ya Rayvanny na mama mtoto wake, Faymah.

Vixen huyo maarufu pia aliwahi fanya kazi na wasanii wakubwa kama vile Mbosso katika wimbo wake wa Hodari, akaja akafanya na Diamond na Rayvanny kwenye wimbo wa Nyegezi ambao ulifungiwa, Lava Lava kwenye ngoma yake ya Go Gaga miongoni mwa nyingine nyingi.

Baada ya ngoma hiyo ya Rayvanny kutoka mnamo mwaka 2019, ilionesha kwenye video mambo ya ukakasi baina ya vixen huyo na Rayvanny ambapo wiki chache baadae mama mtoto wa Rayvanny alipakia picha kwenye mitandao na kusema kwamba mahusiano yake yamekwisha.

Watu walimshtumu pakubwa mwanadada Nana kwamba yeye ndiye kwa asilimia kubwa anayefaa kubebeshwa lawama za kuvurugika kwa penzi la Faymah na Rayvanny.

Mrembo huyo amejitenga na mambo hayo na kusema kwamba ile ilikuwa ni kazi tu na hakuna kingine kilichotokea baina yake na Rayvanny kama ambavyo wengi walikuwa wakihisi.

“Sio mimi. Mimi sikuvunja mahusiano ya Ray na mpenzi wake Faymah ile ilikuwa kazi tu na hata Ray mwenyewe anajua mimi siwezi fanya mambo ya kijinga kwa sababu nipo kwenye mahusiano na mahusiano yangu ni hadharani kwenye mitandao ya kijamii,” Nana alijitenga mbali na madai ya kuvunja mahusiano ya Vannyboy na mama mtoto wake Faymah.

Kwa kuonekana mkweli zaidi, Nana alisema kwamab hata Rayvanny mwenyewe anamjua mpenzi wake na hilo halina mjadala.

Nana aliwataka watu kukoma kumlimbikizia lawana kwamab alivunja mahusiani ya Rayvanny kwani jambo hilo liliwahi kumsababishia athari nyingi sana ambapo alifichua kwamba hadi sasa hivi kichwa kinamuuma kutokana na kuhusishwa na Sakata la kuvunjika kwa mahusiano ya Rayvanny na Faymah.