“Mungu alijua kutakuwa na baridi hii Julai, harafu akanipa Sandra. Raha tupu,” - Akuku Danger

Wawili hao walirushiana maneno wingi jana kwenye mitandao ya kijamii

Muhtasari

• Sandra Dacha alitangaza kwamab yeye na Akuku Danger ni wapenzi wakati mchekeshaji huyo alipolazwa mwishoni mwa mwaka jana.

mchekeshaji Akuku Danger na mpenzi wake muigizaji Sandra Dacha
mchekeshaji Akuku Danger na mpenzi wake muigizaji Sandra Dacha
Image: Akuku Danger (Facebook)

Mchekeshaji Akuku Danger kwac mara nyingine amezuzua mitandao baada ya kuachia ujumbe wa kukanganya kuhusu mahusiano yake na muigizaji bonge, Sandra Dacha, ambaye wiki iliyopita walionekana kurushiana maneno baada ya Danger kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

Mchekeshaji huyo baada ya kuondoka hospitalini, alipakia picha ya pamoja na mwanamke fulani na mtoto, picha iliyosemekana kuwa ni ya familia yake kwa maana ya mke na mtoto.

Picha hiyo ilionekana kutomfurahisha Sandra Dacha ambaye kweney ukurasa wake wa Facebook aliandika maneno yaliyomlenga Akuku Danger huku akimtaka kukoma kupakia picha za mke wake kila mara kwa sababu jambo hilo lilikuwa linamuudhi hata kama alikuwa na ufahamu kwamba yeye ni mpake wake wa kando tu na wala si chaguo la kwanza.

Kwa upande wake naye Akuku Danger alionekana kujibu madai hayo kwa kudokeza kwamba babu yake alikuwa  na wanawake wengi, maneno ambayo wengi walihisi yalikuwa yakimlenga Sandra.

Tangu hapo wambea wa Mitandaoni wamekuwa wakiwafuatilia wawili hao kwa ukaribu ambapo wanasema hawajakuwa wakipakiana kweney mitandao kama kawaida yao. Sandra amekuwa akionekana sana na mchekeshaji Crazy Kennar katika ‘skits’ za mitandaoni huku wengi wakihoji uwepo wa Akuku Danger.

Kutokana na kijibaridi ambacho kimetua katika maeneo mengi ya jiji la Nairobi, Akuku Danger ameachia ujumbe bila picha kwenye Facebook yake alisema kwamba huendqa Mungu alijua baridi ya Julai itakuja na hivyo akampa Sandra mapema. Maneno haya yaliashiria kwamba huenda bado uhusiano wake  na Dacha ungalipo licha ya matukio ya hapo nyuma.

“Mungu alijua kutakuwa na baridi hii Julai, harafu akanipa Sandra. Raha tupu,” aliandika Akuku Danger.

Aidha wengi walihoji ni kwa nini hajapakia picha wakiwa pamoja na Sandra na badala yake kuachia ujumbe mkavu tu.

Dacha alitangaza miezi kadhaa nyuma kwamba yeye na Akuku Danger ni wapenzi, katika kile ambacho alikitaja kuwa ‘Dawa ya balloon siku zote ni Sindano’ akimaanisha yeey kuwa balloon kutokana na umbile lake la kuwa bonge na Akuku kuwa sindano kwa umbile lake la wembamba.