"Unawafunza watoto nini? Kushiriki mapenzi na binamu kabla ya wokovu?" Kibe amponda Kabi

Kibe alimponda Kabi na kusema kwamba suala kama hilo si la kujigamba nalo tena mbele ya umati wa waumini.

Muhtasari

• Kabi wa Jesus wikendi iliyopita alizungumza kwamba alishiriki kitendo na binamu zake wengi  na wala si yule mmoja anayejulikana.

Kabi wa Jesus na Andrew Kibe
Kabi wa Jesus na Andrew Kibe
Image: YouTube (Screenshot)

Mkuza maudhui wa mtandao wa YouTube, Andrew Kibe amemkashfu vikali mkuza maudhui mwenzake Kabi wa Jesus wa kuweka wazi mbele wa umati wa waumini kwamba aliwahi fanya mapenzi na binamu zake zaidi ya mmoja.

Kulingana na Kibe, kitendo cha Kabi wa Jesus kusema ukweli wa maisha yake ya nyuma mbele ya umati wa waumini ni kama kumdhalilisha mke wake Milly wa Jesus.

Kabi wa Jesus wikendi iliyopita katika moja ya ibada za kanisani aliamua kuzungumzia kitendo kilichotokea mwaka jana ambapo mmoja wa binamu zake aliweka wazi kwamab waliwahi shiriki kitendo cha ngono na Kabi na mpaka kuzaa mtoto pamoja, tukio lililogonga vichwa vya habari haswa baada ya matokeo ya DNA kuonesha kwamab mtoto yule ni wa Kabi wa Jesus.

Kabi aliweka wazi kwamba ni kweli wengi wanajua mtoto yule ni wake kutokana na Sakata hilo la mwaka jana lakini wasilolijua ni kwamba aliwahi kushiriki kitendo cha ngono na wengi wa binamu zake na kile kisa kimoja kwenye meza ya umma ni kama tu tone la ufuta kwenye bahari.

“Kabla sijapata wokovu suala la kushiriki kitendo na binamu zangu halikuwa  suala na yeye hakuwa wa kwanza. Nimelala na wengine wengi sana, unazungumzia nini? Mwenye alipata mimba huyo tu nido mnajua, asifiwe Bwana,” alisema Kabi mbele ya umati wa cwauminic waliojawa na mshangao.

Maneno haya ya Kabi hayakuenda sawa na Kibe ambaye kupitia ukurasa wake wa YouTube amemponda Kabi vikali na kusema kwamba hakufaa kusema hivo mbele ya umati wa kanisa na kusema hivo ni kama kumshushia heshima mkewe katika macho ya kanisa.

Kibe alitema lulu kwa kusema kwamba watu wengi katika usasa huu wamekuwa wakilizungumzia suala la kufanya ngono na watu wa ukoo, jambo ambalo kulingana na yeye linapotosha jamii na linafaa kukemewa vikali, na wala sio kulizungumzia mbele ya umati wa waumini kama njia moja ya kutanua kifua na kutamba arijojo.

Kibe alisema kwamba Kabi kuzungumza kanisani ambapo pia kuna hadi watoto ni kaam kuwqafundisha kwamba kabla ya kupata wokovu, mtu unweza fanya kitendo hicho na watu wa ukoo na kukiacha baada ya kupata wokovu.