(Video) Bien Aime, Nick Mutuma wamkaribisha Magix Enga chama cha vipara baada ya kunyoa rasta

Magix Enga alipakia video akinyolewa rasta zake.

Muhtasari

• Mzalishaji  huyo mwenye utata alionesha akiwa kichwa upara baada ya kukata rasta zake za muda mrefu.

Mzalishaji maarufu nchini wa miziki ya kiduni, Magix Enga hatimaye amenyoa ‘rasta’ zaka ambazo kwa muda mrefu zimekuwa kama nembo ya utambulisho wake.

Kupitia Instagram yake, Enga amepakia video akiwa kweney kinyozi ambapo rasta zote zimekatwa na kuwekwa juu ya kimeza na kuifuatisha video hiyo kwa maneno kwamba “Kichwa safi kama balloon”

Watu wengi hawajaamini kama ni kweli msanii huyo mwenye utata amekata rasta zake kutokana na kile walitaja kwamba msanii Diamond pia kipindi cha nyuma akitoa albamu yake nusu ya FOA aliwahi pakia video ikimuonesha kanyoa upara kumbe ni uongo ulikuwa ni uhariri tu katika video ile.

Huyu si mtu wa kwanza kukata rasta zake ambapo miezi kadhaa nyuma mkuza maudhui wa YouTube, Thee Pluto pia alipakia picha akiwa amekata zake ambapo alisema kwamab ni Rafiki yake alimuahidi kiasi fulani cha pesa kaam atazikata, na kwa kuwa hangetaka kupoteza ahadi ile ya pesa basi akazikata.

Vile vile mjukuu wa rais hayati Mwai Kibaki, Sean Andrew alikata zake mwezi mmoja tu kuelekea kifo cha babu yake ambapo kwa upande wake alitoa sababu kwamba ni dhana potovu dhidi ya watu wenye rasta ndio ilimfanya akaondokea chama hicho.

Magix Enga hajatoa sababu za kunyoa nywele zake kama ni kweli amezikata ia wasanii mbali mbali wenye mtindo wa kunyoa upara wamefurika kwenye ukurasa huo wa Instagram na kumpongeza kwa kujiunga chama chao huku wakimkaribisha kwa mbwe mbwe.

Msanii Bien Aime wa kundi la Sauti Sol amemkaribisha kwa kumpigia makofi, Barasa ni mmoja wa watu wenye kunyoa upara ambapo hadi wamefanya wimbo wa kusifia wanaume wenye vipara.

Mtayarishaji wa filamu maarufu Nick Mutuma ambaye pia ni mtu wa chama cha vipara pia amempongeza na kumkaribisha kweney kundi.

“Karibu kwenye maisha matamu,” aliandika Mutuma.