Jamaa kutoka Busia adai kuwa mwanawe Vera Sidika

Jamaa huyo ambaye ni mchekeshaji alitaka kushirikishwa katika sherehe za kuchipuka jino la kwanza la Asia Brown

Muhtasari

• “Mimi kitu tu naomba kutoka kwa Vera ni anipe tu nafasi moja ya kuzungumza na yeye, hata kaam ni dakika moja" - Jamaa huyo alisema.

Jamaa mmoja kutoka kaunti ya Busia kwa mara nyingine tena amejitokeza wazi kudai kwamba yeye ni mtoto halali wa mwanasosholaiti Vera Sidika.

Jamaa huyo anayejitambulisha kama Handsome Boy anataka aruhusiwe kushiriki katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa na bintiye Vera na Brown Mauzo, Asia Brown ambaye sasa anadai ni kama dada yake mdogo.

Akifanyiwa mahojiano na mwanablogu mmoja wikendi iliyopita, mwanaume huyo alimuomba Vera amkaribishe kwenye sherehe za kusherehekea kuchomoza kwa jino la kwanza la Asia Brown, sherehe ambayo Vera alidokeza wikendi iliyopita kwamba huenda ataiandaa.

“Siogopi kusema Vera, mimi ni mtoto wako. Nimesikia mamangu ako na party ya dadangu, najiuliza, kwani hiyo party anamfanyia ya kuchipuka kwa jino la kwanza si hata mimi anifanyie ama anikaribishe nione hata dadangu,” Jamaa huyo alisema bila kutetereka.

Jamaa huyo alisema kwamba mara ya mwisho walionana na Vera Sidika katika kaunti ya Kakamega ambapo mwanasosholaiti huyo alimtelekea kabla ya kuja jijini.

Hii si mara ya kwanza kwa mwanaume huyo kujitokeza wazi na kudai kwamba Sidika ni mamake, ambapo Vera alipuuzilia mbali madai hayo na kusema kwamba kwa muonekano wenyewe mwanaume huyo anaonekana kuwa mkubwa kumliko ambapo alimtaja kuwa huenda alizaliwa hata yeye mwenyewe kuzaliwa hali ya kuwa anasema sasa yeye ni mamake.

Kwa upande wake mwanaume huyo anazidi kusisitiza kwamba Sidika ni mamake wa kumzaa na anataka hata yeye afanyiwe sherehe za kusherehekea meno yake 32 ambapo alifichua kwamba hata mengine tayari yashaanza kung’oka na hajawahi fanyiwa sherehe hali ya kuwa dadake anaandaliwa sherehe kwa kuchomoza kwa jino la kwanza.

“Mimi kitu tu naomba kutoka kwa Vera ni anipe tu nafasi moja ya kuzungumza na yeye, hata kaam ni dakika moja nizungumze na yeye uso kwa uso nimwambie ni nini natafuta kwa maisha yake,” mwanaume huyo aliomba Vera kumsikiza.