"Kwani Nandy ni benki?" Billnass ajibu madai kwamba alifuata Nnandy juu ya pesa na wala si mapenzi

Wawili hao walivishana pete za uchumba Februari mwaka huu nyumbani kwao Nandy.

Muhtasari

• Billnass alisema yeye hajawahi muona Nandy kama mtu mwenye pesa na kusema tatizo lipo kwa wenye wanamuona hivo.

Wasanii na ambao pia ni wachumba, Billnass na Nandy
Wasanii na ambao pia ni wachumba, Billnass na Nandy
Image: INSTAGRAM

Msanii na mjasiriamali wa kampuni ya kuuza vifaa vya umeme ya Nengatronix, Billnass amekanusha vikali madai kwamba aliingia katika mahusiano na mwanamuziki Nandy kwa ajili ya utajiri wa malkia huyo wa muziki.

Akizungumza na wakuza maudhui wa mitandaoni, Nenga kama anavyojiita alisema hawezi mwambie mtu anayesema chochote kwa sababu siku zote wenye midomo lazima tu wataongea kwa sababu hiyo ndio kazi ya mdomo haswa.

“Kwani Nandy ni benki? Mimi sina chochote cha kumwambia mtu anayesema chochote kwa sababu kila mtu ana huru wa kusema kile anachofikiri kwa namna yake. Pia mtu akiona Nandy ana pesa sana hiyo ina maana huyo ni maskini sana kwa sababu mimi sijawahi ona Nandy kama ana pesa sana,” Billnass alisema.

Msanii huyo pia alisisitizac kwamba tatizo lipo kwa yule anayeliona hivyo kutokana na kipato chake kwani yeye hawezi eti ameacha mambo yake yote na kuanza kumfuata mwanamke kwa sababu ya pesa na mali zake. Alisema siku zote yeye hajawahi kuuona Nandy kama Tajiri au mtu mwenye pesa kama watu wengine wanavyomuona.

Billnass alifunguka kwamba kama mwanandoa yeyote baada ya harusi kukamilika anatamani kuwa na familia ila akampa Mwenyezi Mungu nafasi kubwa kwa kusema kwamba ataikubali Kamba ambavyo Muumba atakavyoiratibu.

Pindi baada ya kuweka wazi mahusiano yake na mwanamuziki Nandy, watu wengi walitoa hisia zao waking’aka kwamba mwanamuziki huyo wa muda mrefu alizama kwenye penzi la Nandy si tu kwa sababu alikuwa na mapenzi ya dhati ila kwamba alikuwana njama ya kushusha kitonga kusafiria nyota ya Nandy.

Nandy na Billnass walivishana pete za uchumba mwezi Februari mwaka huu na pia hivi majuzi wametangaza kufunga ndoa ya kifahari ambayo mwenyekiti wa kamati nzima ya kusimamia shughuli za arusi atakuwa muigizaji Steven Nyerere.

Wiki iliyopita Nyerere alitangaza kwamba harusi hiyo itakuwa kubwa mpaka kuweka wzi kwamba kamati inafikiria kuuliza ridhaa kwa mamlaka kutangaza siku ya harusi kuwa siku kuu ili kumpa kila shabiki wa wasanii hao kuhudhuria ama kwa njia ya moja kwa moja runingani au kufika mazima katika eneo la tukio hilo la kihistoria.