Mwanamke aiandikia mahakama barua akimtetea R Kelly, asema walikuwa wachumba

Muhtasari

• Mwanamke huyo alisema serikali imekuwa ikimuonesha kuwa mwathiriwa wa vitendo vya kinyama vya R Kelly.

• Amesisitiza kwamba hakuwa mwathiriwa wake bali mchumba wake na walikuwa wanapendana.

Msanii mkongwe R Kelly na mwanamke anayedqai kuwa mpenzi wake, Joycelyn Savage
Msanii mkongwe R Kelly na mwanamke anayedqai kuwa mpenzi wake, Joycelyn Savage
Image: Twitter

Mmoja kati ya wathiriwa wa vitendo vya kinyama vya msanii wa Kimarekani R Kelly kwa jina Joycelyn Savage amejitokeza wazi na kumtetea mwanamuziki huyo huku akisema kwamba walikuwa wachumba.

Katika barua ambayo ilisambazwa mitandaoni juzi, Savage anaonekana kumtetea mwanamuziki huyo mkongwe na mpaka kumtaka hakimu kumpunguzia hukumu kwani alikuwa anampenda sana.

Mwanamke huyo ambaye awali alikuwa anatajwa kuwa mmoja kati ya wathiriwa vya vitendo vya kinyama vya R Kelly alisema kwenye barua hiyo kwamba anataka kumtetea Kelly na hata kuiambia mahakama ukweli kwamba hakuwa mwathiriwa kama ambavyo mahakama imekuwa ikimuita bali walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Kelly na mpaka kuchumbiana.

“Jina Langu ni Joycelyn Savage, mimi ni mchumba wa Robert Kelly. Ninaandika barua hii kwa utetezi wa Kelly mbele kabla ya hukumu rasmi kutolewa ili kwamba nipate nafasi ya kutoa Ushahidi wangu kwa korti kwamab mimi si mwathirika wa vitendo vyake kama ambavyo serikali imekuwa ikinielezea,” sehemu ya barua hiyo ilisoma.

Mwanamke huyo alizidi kuelezea kwa mambo makubwa yaliyostua ulimwengu uliofikiwa na barua ile kwa kusema kwamba uhusiano wake na R Kelly ulikuwa wa kusisimua mno na mpaka kumtaja kuwa ‘ni kitu kizuri zaidi kuwahi kutokea katika maisha yangu’

“Tuna mahusiano yenye yameunganika pakubwa na tumezama katika kina kirefu cha mapenzi. Mimi namtetea Kelly mpaka dakika hii kwa sababu nilikuwa nampenda na bado nampenda na nitakuwa hapa kusimama na yeye. Kelly si janabi ambalo serikali imemuelezea kuwa. Namjua ni jamaa mpole, mnyenyekevu na mtamu kwa sababu mwisho wa siku alikuwa anahakikisha kwamba mahitaji yangu yamekidhiwa, pamoja na wanawake wengine ambao aliwahi kuwa nao pia,” Mwanamke Savage aliamua kusema ukweli kwenye barua ile.

Image: Twitter

Mwanamke huyo aliyeonekana kuzama kabisa katika dimbwi la mapenzi ya Kelly alisema kwamba inamuuma sana kuona kwamba serikali imeweka picha ya Kelly vichwani mwa watu kama mtu mbaya asiyestahili nafasi katika jamii na kusema kwamba Savage ni mwathiriwa wa vitendo vyake, jambo ambalo amelikanusha vikali.

“Mimi basi ninaiomba mahakama kuzingatia maneno yangu wakati wa kutoa hukumu kwa Robert Kelly. Ni mwanaume mzuri mwenye moyo mkubwa na anastahili kuwa nyumbani kujumuika na wapendwa wake ambao wako tayari kabisa kusimama na yeye,” Joycelyn Savage alimalizia barua yake.