Maoni: Diamond amelainisha muziki wa Bongo, kama unamdharau maanake unavuta bangi

" Huyu jamaa ni wa kiwango kingine kabisa, jamaa ana akili kama Ruge,"

Muhtasari

• "Kama hautambui mchango wa Diamond basi sio siri utakuwa ni mvuta bange akili zako hazijakurudi,”

Diamond na Harmonize
Diamond na Harmonize
Image: Screengrabs: YouTube

Mwanablogu mmoja nchini Bongo amekuja ya mapya ambapo sasa anasema mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kabisa kumdharau ama kumzushia bifu msanii Diamond Platnumz kwani yeye ana akili nyingi kuliko wasanii wote waliowahi kutokea katika ardhi ya taifa hilo tangu uhuru miaka ya sitini.

Kupitia kweney ukurasa wa Instagram ambapo maneno haya yalitokota kwa mjadala mkali, mwanablogu huyo alidai kwamba Diamond si mtu wa kawaida kwamba wengine waanze kumchukulia poa kwani yeye ana moyo tofauti kabisa katika kusaidia.

Alimfananisha msanii huyo kuwa wa uelewa mkubwa wa Sanaa kama marehemu mtangazaji nguli Ruge, na kusema mpaka sasa wengine wanachokifanya kimuziki ni kuiga tu mambo ambayo Diamond amefanya kwa miaka zaidi ya kumi ambayo amekuwa katika Sanaa.

“Kama una akili timamu huwezi ukamchukulia poa Diamond Platnumz. Huyu jamaa ni wa kiwango kingine kabisa, jamaa ana akili kama Ruge, yeye ndiye amelainisha muziki wa Bongo Fleva, hivi sasa vijana wote wanafanya kwa kumuiga yeye,” aliandika.

Mshika dau huyo katika sekta ya muziki pia alisema Diamond ndiye mtu pekee mweney moyo wa kumtoa mtu kijijini mwao na kumleta mjini kumsaidia kimaisha, akitolea mfano msanii Harmonize ambaye alikuwa hovyo kabla ya Diamond kumshika mkono na kumfanya kutusua kimuziki.

Pia alisema msanii Rayvanny kabla ya kuingia WCB alikuwa kabwela wa kutupwa mara kumi ila baada ya Diamond kumshika mkono alifanikiwa kuwapata warembo na kina Paula na Fahyvanny ambao ni pisi kali kupindukia.

“Aisee kama wewe ni mtanzania na hautambui mchango wa Diamond basi sio siri utakuwa ni mvuta bange akili zako hazijakurudi,” mwanablogu huyo alisema.