Iyanii na Harmonize watarajiwa kutoa collabo, remix ya Furaha

Iyanii aliingia kwenye gemu mwishoni mwa mwaka jana na kibao chako cha ' pombe'

Muhtasari

• Hii itakuwa collbao ya pili mwaka huu kwa msanii Harmonize kushirikishwa na msanii kutoka kenya.

Wasanii wa kizazi kipya Iyanii na Harmonize, wanatarajiwa kutoa collabo yao Jumatatu.
Wasanii wa kizazi kipya Iyanii na Harmonize, wanatarajiwa kutoa collabo yao Jumatatu.
Image: Instagram

Msanii wa kizazi kipya anayechipukia kwa kasi mno nchini Kenya, Iyanii anatarajiwa kuachia kibao chake cha moto amabcho amemshirikisha staa wa Tanzania Harmonize Platnumz.

Akitangaza taarifa hizi njema kwa wapenzi wa muziki wa Kenya, Iyanii aliandika kwenye Instagram yake kwamba Jumatatu hii collabo hiyo ambayo ni remix ya ‘Furaha’ ngoma yake ya pili kwenye gemu la muziki wa Kenya.

“Tayarisha viatu vyako vya kucheza densi siku ya JUMATATU ndio siku kuu. Iyanii ft @harmonize_tz. Niamini hii itakuwa kubwa na nzuri ajabu,” Iyanii aliandika.

Meneja wa Harmonize ambaye nia ni mpenzi wake, Fridah Kajala Masanja pia alidhibitisha taarifa hizi kwa kusema kupitia instastory yake kwamba mumewe Harmonize anatarajiwa kuachia collabo yake na msanii Iyanii.

Iyanii ambaye aliibuka kwenye Sanaa ya muziki wa Kenya mwishoni mwa mwaka jana na ngoma yake iliyopata mapokezi makubwa kwa jina ‘Pombe’ amekuwa akifanqay vizuri ambapo remix hiyo ni kutoka kwa ngoma yake ya pili tangu ujio wake, aliposhikwa mkono na msanii Arrow Bwoy.

Msanii huyo yuko katika ziara za amani na kuutambulisha muziki wake zaidi nje ya mipaka ya nchi ambapo wiki jana alikuwa ziarani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kabla ya kutimba Tanzania alikokutana na mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide, Harmonize na maelewano ya kutoa remix ya Furaha yakazaliwa.

Kwa upande wake Harmonize, hii itakuwa ngoma yake ya pili mwaka huu akishirikishwa na Mkenya ambapo ya kwanza kabisa ilikuwa ile ya ‘Woman’ akishirikishwa na msanii matata Otile Brown, ngoma ambayo kwa miezi mitano sasa imefanya vizuri kwenye majukwaa mbali mbali ya kupakua miziki ndani na nje ya nchi.