"Rafiki yako ako 24 na anaendesha Mercedes, usishawishike, labda ni mwizi" Abel Mutua ashauri

Abel Mutua alisema usitake kuwa tajiri kama rafiki zako wa rika sawa kwani huwezi ukajua chanzo cha utajiri wao

Muhtasari

• Mutua aliwataka watu kuwa na subira kwani kila mtu ana muda wake mwafaka wa kufanikiwa maishani.

Muongozaji wa filamu humu nchini Abel Mutua
Muongozaji wa filamu humu nchini Abel Mutua
Image: Instagram//Abel Mutua

Muongozaji maarufu wa filamu nchini Kenya Abel Mutua kwa mara nyingine tena ametema lulu zake katika kutoa ushauri nasaha kwa vijana wanaokumbwa na shinikizo la kutaka kufaulu kwenye maisha.

Katika video fupi ambayo imesambazwa kweney mitandao ya kijamii, Mutua anawaambia vijana kuwa na Subira katika maisha na kamwe kutosogezwa au kutojawa na shinikizo baada ya kuona wenzao wenye rika sawa nao wamefaulu maishani.

“Rafiki yako ako na miaka 24 na anaendesha mercedez baridiii! Pia wewe unataka kusombwa na shinikizo hapo na mtu ni mwizi. Hujui huyu jamaa hili gari amelipata kwa njia gani,” Mutua alisema.

Pia alizidi kuhimiza na kusema kwamab katika maisha, hakuna ushindani kwani kila mtu ana muda wake aliopangiwa na Mungu kufanikiwa.

“Rafiki yangu, polepole. Muda wa kila mtu ni tofauti. Wewe utafanikiwa ukiwa 25, mwenzako atafanikiwa akiwa 18, mwingine atafanikiwa akiwa 40. Hakuna makosa ilmradi ubaki mkweli kwa nafsi yako,” alisema Abel Mutua.

Aliwataka watu kukoma kuona watu wengine wenye wamefanikiwa kuwa wamepitia njia rahisi na kupata hiyo mali wanayomiliki.

Mutua anasema si kila mtu unayemuona kweney mitaa akiwa na utajiri ameupata kwa njia halali kwani wengine licha ya kuwa na utajiri huo bado wanaishi kwa wasiwasi mkubwa kila mara wapo kama kunguru anayekimbilia maisha yake kwa kuogopa kufuatwa na waliowadhulumu.

“Hawa watu wakakwambia ukweli vile wamepata vitu vyao, utashtuka. Utapa kwamba licha ya wao kuwa matajiri, wewe unaishi maisha mazuri ya amani kuwaliko kutokana na wao kuishi maisha ya kuangalia nyuma kila wakati kwa mashaka juu wanaogopa wanaweza kuwa wanafuatwa na watu,” Mutua alisema.

Muongozaji huyo wa filamu ameonekana akitoa ushauri uliokolea kwenye mitandao siku za hivi karibuni ambapo wiki jana aliwashauri watu kufuatilia mambo yao zaidi badala ya kushinda wakimrai yeye na mke wake kupata mtoto wa pili. Alidokeza kwamba hana mpango wa kupata mtoto wa pili hivi karibuni na wale wote wanaomtaka azae mtoto wa pili basi watakuwa wamebugi stepu.