"Unataka nikonde unipeleke wapi?" Sandra Dacha awasuta wanyanyapaaji mitandaoni

Muigizaji huyo mwenye umbile kubwa anajivunia muonekano wake lichqa ya kuburuzwa katika mitandao ya kijamii.

Muhtasari

• Alifichua kwamba yeye alianza kunyanyapaliwa mitandaoni kitambo na sasa amezoea

Muigizaji Sandra Dacha akiwa amejiweka vizuri kwa ajili ya picha
Muigizaji Sandra Dacha akiwa amejiweka vizuri kwa ajili ya picha
Image: Facebook//Sandra Dacha

Muigizaji Sandra Dacha amechemkia kama mvinyo wa kiasili uliotiwa chachu wambea wanaomsimanga kwenye mitandao ya kijamii kuhusu maumbile ya mwili wake bonge.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Dacha aliwataka wote wanaoyasema maumbile yake kumkoma kwani mwisho wa siku wanataka akonde ili wampeleke wapi.

Ati nimemona sana. Unataka nikonde unipeleke wapi?” Sandra Dacha aliuliza wenye nongwa.

Mwanamama huyo ambaye kwa muda mrefu ameonekaan kujikubali jinsi alivyoumbwa na hata kujibandika jina la kimajazi kama mashine kubwa wiki juzi katika mahojiano ya moja kwa moja kwenye kituo kimoja cha redio humu nchini alisema kwamba yeye alianza kujikubali kitambo sana enzi akiwa shule ya upili na sasa hivi wala hababaishwi na maneno ya watu kuhusu umbile lake kwani amezoea.

Kulingana na yeye, wale wanaousema mwili wake wa kibongebonge wanajichosha bure kwani wanadhani wanamkomoa kumbe ndio mwanzo wanamjaza ujasiri wa kujiamini na kujikubali zaidi ya kila kitu.

Kwa waaki fulani Dacha ambaye alifichua kwamba yeye na mchekeshaji Akuku Danger si tu marafiki bali pia ni wapenzi, aliwahi jilinganisha na puto na kusema kwamba kutokana na wembamba wa mchekeshaji Akuku Danger, basi ndiye dawa yake, msemo ambao ulizungumziwa sana mitandaoni kwamba ‘dawa ya puto ni sindano’

Baada ya kuletana juu na Akuku kuhusu mcheshi huyo kupakia picha za mara kwa mara mitandaoni za mke wake wa kwanza na mtoto wake, Dacha alikuja baadae akalainisha mambo na kusema kwamba yeye na Akuku wala hawana mpango wa kuachana muda wowote hivi karibuni na kuwaambia wanakamati wa roho chafu kwamba iwapo walitegemea watengane basi wameula wa chuya.