(Video) Jamaa amabaye sura yake imekuwa ikitumika kama 'meme' ya kulia azungumza

Jamaa huyo alisema alipokuwa akilia hajui nani alichukua pichqa yake na baadae kuisambaza kote ulimwenguni kama meme

Muhtasari

• "Kwa hiyo siku hiyo nyanya alinipa N200 ili kununua chakula cha jioni, nikapitia kwa marafiki nikacheza kucheza kamari nikapoteza" - Jamaa huyo alisema.

Kijana ambaye picha zake akilia zimekuwa zikitumiwa sana nchini Kenya kama meme ameelezea nini kilichotokea siku ambayo alichukuliwa kwenye video na picha akilia.

Kulingana na kijana huyo kutoka Nigeria, alisema kwamba alitumia pesa za nyanya yake kuwekeza katika michezo ya bahati nasibu ila hakupata bahati ya kushinda kama alivyokuwa akidhania.

Mwanaume huyo mbilikimo mwenye muonekano wa kuchekesha alisema kwamba alipoteza pesa hizo kwenye mchezo wa kuwekeza ambapo alikuwa anategemea kushinda na kilio kile kilitokana na vile alipokuwa akitafakari jinsi ya kukwepa adhabu kali kutoka kwa nyanya yake.

Kijana huyo ambaye jina lake bado halijawekwa wazi kwa umma alisema siku hiyo nyanyake aslimpa pesa za Kinigeria 200 ambazo ni sawa na shilingi 55 pesa za benki kuu ya Kenya ili aende kununua chakula cha usiku lakini akapitia kwenye kichochoro cha duka la ubashiri kujaribu bahati yake ya kutengeneza faida ya haraka.

“Kitu kilichotokea siku ile unajua kwanza mimi naishi na nyanya yangu kijijini. Na wakati huo kupata angalau kitu kidogo kijijini inakuwa ngumu sana kwa namna fulani. Kwa hiyo siku hiyo nyanya alinipa N200 ili kununua chakula cha jioni, nilipokuwa naelekea dukani nilipitia kwa rafiki yangu kucheza mchezo wa bahati nasibu, baadae nilipoteza mchezo ule kwa rafiki zangu na pesa wakazichukua,” Kijana huyo anasikika akieleza kwenye video moja iliyopakiwa kwenye ukurasa wa Instagram wa Gossip Mill.

 Kijana huyo alisema hajui ni nani wala nis aa ngapi alipigwa picha ile ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikitumiwa mitandaoni kaam kioja cha kuchekesha kutokana na jinsi alivyokunja uso kwa hamaki kubwa.