"Huyu ni mtoto wa kimiujiza, nilimzaa na miezi 6, kheri njema ya kuzaliwa" - Kathy Kiuna

Mchungaji Kathy Kiuna alimsherehekea mwanawe Jeremy Kiuna siku yake ya kuzaliwa na kusema alimzaa kabla ya ujauzito kutimia.

Muhtasari

• “Kicheko hicho cha moyo unachokiona kinatoka mioyoni mwetu. Furaha ya Bwana imekuwa nguvu yetu." - Kathy Kiuna

Mchungaji Kathy Kiuna wa kanisa la JCC akimsherehekea mwanawe Jeremy Kiuna siku yake ya kuzaliwa.
Mchungaji Kathy Kiuna wa kanisa la JCC akimsherehekea mwanawe Jeremy Kiuna siku yake ya kuzaliwa.
Image: Facebook///Kathy Kiuna

Mchungaji Kathy Kiuna amemsherehekea mtoto wake wa kiume kwa jina Jeremy katika siku yake ya kuzaliwa na kumtaja kuwa baraka kubwa katika maisha ya familia hiyo ya walokole.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, mchungaji Kathy Kiuna alisema mtoto huyo ni kitu cha ajabu sana kaam vile muujiza kwani alizaliwa kama njiti – alizaliwa miezi mitatu kabla ya ujauzito kutimia.

Kiuna alisema kwamab kumuona mtoto huyo akikuwa kutoka kuzaliwa akiwa na miezi sita, kukua na kumaliza shule ya upili na alama ya A imara pamoja na kuhitimu kutoka chuo kikuu hivi majuzi ni zaidi ya baraka tele na mfululizo.

“Ni siku ya kuzaliwa ya mwanangu. Jeremy ni mtoto wa ajabu aliyezaliwa akiwa na miezi 6. Kila hatua aliyopiga maishani ni kubwa. Kumwona akiwa mwanafunzi wa A moja kwa moja na amehitimu hivi karibuni kutoka chuo kikuu kunasisimua tu sana,” aliandika kwa furaha Mchungaji Kiuna kwenye Facebook.

Alipakia picha ya pamoja wakiwa wamekumbatiana na mwanawe huku nyuso zao zikiwa zimesheheni tabasamu la kudumu na kusema kwamab furaha hiyo mnayoiona kweney uso wa mwanawe ni kutoka nyoyoni mwao na pia akasema Jeremy atazidi kukua katika misingi dhabiti katika Mungu.

“Kicheko hicho cha moyo unachokiona kinatoka mioyoni mwetu. Furaha ya Bwana imekuwa nguvu yetu. Jeremy ni mtoto wa kusudi na atafanya mambo makuu kwa ajili ya Mungu. Tazama nafasi hii. Tafadhali nisaidie kumtakia siku njema ya kuzaliwa Jeremy Kiuna. Ninakupenda zaidi kuliko maneno yanayoweza kusema. Furahia siku hii na miaka mingi mbele asali,” alisema Kiuna.

Kathy Kiuna na mumewe Allan Kiuna ndio wanaongoza kanisa la Jubilee Christian C      hurch lililoko katika barabara kuu ya Thika na mhubiri huyo aliwahi zungumzia hadithi yake na ujauzito wa Jeremy ambapo wakati mmoja kwenye video aliyoipakia YouTube alielezea kwamba mimba hiyo ilikuwa na matatizo na madaktari walimtaka kuiavya ila akakataa katakata na kuilea licha ya kuambiwa matatizo yaliyokuwa yakisababishwa nayo.