(Video) "Kila mtu abebe mzigo wake" Boniface Mwangi abebwa mgongoni na mkewe

Miezi minne iliyopita, Boniface Mwangi na mkewe walikuwa wanasherehekea miaka 14 tangu waoane.

Muhtasari

• Mwangi alisema video hiyo ilionesha jinsi walikuwa wakifanya mazoezi wakati wa kafyu ya Corona.

Mwanaharakati wahaki za kibinadamu Boniface Mwangi ameacha wengi katika kicheko kikubwa baada ya kupakia video kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akiwa amebebwa mgongoni na mkewe, Njeri.

Katika video hiyo Mwangi anasema ndio jinsi walivyokuwa wakifanya mazoezi na mke wake kipindi nchi iliwekewa kafyu na kufungwa kutokana na msambao wa virusi vya janga la Corona.

Alimsifiwa mkewe kwamba anayeonekana na barakoa na kusema kwamab kipindi hicho ilikuwa ni marufuku mtu kutoka nje bila moja na pia akasema mkewe anajua kweli kubeba uzito wa aina yote na si tu ujauzito.

“Jinsi tulivyokuwa tukifanya mazoezi wakati wa kufungwa kwa nchi kutokana na Covid-19. Ilikuwa ni hatia kuondoka nyumbani kwako bila barakoa. @njerikan anajua kubeba uzito,” Boniface Mwangi aliandika kwenye Instagram.

Njeri anaonekana akihema huku akitembea na Boniface Mwangi mgongoni mwake kama mtoto huku Mwangi anaaachia tabasamu mpaka jino la mwisho.

“Kila mtu abebe mizigo yake,” Mkewe Mwangi anasikika akisema huku wanatembea kaam njia moja ya kufanya mazoezi kulingana na maneno ya mwanaharakati huyo ambaye alikuwa mwanahabari mpiga picha.

Mwangi katika filamu yake ya Softie aliwahi kuelezea jinsi ambavyo walikutana na mkewe ambaye pia alikuwa mwanaharakati kipindi cha vurugu za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007-08 ambapo Mwangi alikuwa mpiga picha, picha ambazo zilimshindia tuzo kubwa.

Mwangi alisema kwamba walikutana na Njeri kipindi hicho ni miaka michache baadae waakfunga ndoa takatifu ambapo mpaka sasa wamedumu katika ndoa yao.

Mwangi alijaribu bahati yake katika siasa za eneo bunge la Starehe mwaka 2017 ambapo alipoteza kwa mbunge wa sasa Charles Njagua.

Kwa sasa Mwangi alisema hana haja ya kuwania tena na badala yake amejibwaga nyuma ya mgombea urais Raila Odinga na mgombea mwenza wake Martha Karua ambaye ni mwandani mkubwa wa Mwangi na inaarifiwa alikubali kunadi sera za Raila kutokana na uteuzi wa Karua kama mgombea mwenza wake kuelekea uchaguzi wa Agosti ambao ni wiki tatu zijazo.