Rayvanny anunua pombe ya Tsh 4M kusherehekea collabo na Mualbania

Ijumaa Rayvanny aliachia collabo ya Pele Pele na Mualbania Luana Vjollca

Muhtasari

• “Maison, haya mambo mimi nilikuwa sitaki jamani, milioni tano ya nini sasa,” Rayvanny anasikika akiteta.

Msanii wa bongo fleva Rayvanny
Msanii wa bongo fleva Rayvanny
Image: Instagram//Rayvanny

Mapya kabisa kutka nchini Tanzania ni kwamba msanii mkurugenzi mpya kabisa nchini humo wa lebo ya kutengeneza na kurekodi miziki, Rayvanny amesemekana kununua pombe kwa kiasi kikubwa kabisa cha pesa kuwahi kutokea kwenye ardhi ya Tanzania tangu uhuru miaka ya sitini.

Ijumaa Rayvanny aliachia ngoma yake ambayo ni collabo na msanii wa kimataifa kwa jina Luana Vjollca kutoka taifa la Albania, kibao kinachokwenda kwa jina Pele Pele ambamo usiku wa kuamkia leo aliamua kurusha tafrija la aina yake katika kumbi moja ya starehe jijini Dar es Salaam kwa jin Maison.

Katika usiku huo wa tafrija ndio inasadikika Rayvanny alimwaga pesa kwenye vilevi kwa mashabiki wake wengi waliojitokeza kusherehekea na yeye collabo ya kwanza na msanii kutoka Albania, msanii wa kwanza Afrika mashariki kuwahi kufanya collabo na msanii kutoka taifa hilo, hata Diamond Platnumz mwenyewe aliyemlea Rayvanny hakuwahi fanya collabo na msanii kutoka AlbanIA.

Kwenye instastories zake, Msanii Rayvanny anaonekana na kusikika akizungumza na msanii chawa wa wasafi, Baba Levo ambaye anamuuliza mbona akakubali kununua pombe kwa kiasi ghali namna ile.

“Maison, haya mambo mimi nilikuwa sitaki jamani, milioni tano ya nini sasa,” Rayvanny anasikika akiteta.

“Wamekukomesha ndugu yangu, milioni 5.8. kumbe kununua pombe inaletwa na watu wamebeba kwa kusherehekea, kumbe ni chupa ndogo inauzwa milioni 4, aah wale ni mashetani,” Baba Levo anaonekana akikemea pia.

Rayvanny aliachia kibao hicho chake cha PelePele siku chache tu baada ya kuondoka WCB huku wengine waking’aka kwamab kuondoka kwake ndio kama amejichimbia kaburi kwani hatotusua tena kimuziki, lakini ni kama Rayvanny yumo mbioni kuwakomesha wote waliotilia shaak kuondoka kwake na kujijenga upya na lebo yake ya Next Level Music.