Karen Nyamu: Ninavalia nguo za kujifunika juu mpaka chini ili kupata mtu wa kunitolea mahari

Karen alikuwa akizungumza kwa utani huko kaunti ya Nyandarua siku chache zilizopita.

Muhtasari

• Karen Nyamu ana watoto wawili, mdogo akisemekana kuzaa na mwanamuziki wa Mugithi, Samidoh.

Image: Instagram//KarenNyamu

Mwanasiasa Karen Nyamu akiwa katika kampeni za kumpigia debe naibu rais William Ruto kwenye kaunti ya Nyandarua wikendi iliyopita alichekesha watu baada ya kusema kwamab siku hizi anavalia nguo za heshima ili kuvutia mwanaume wa kumuoa.

Nyamu alivunja mbavu kwa utani kwamba anavalia nguo za kuufunika mwili wake wote ili angalau kufurahisha mwanaume mwenye atakayemtolea posa.

“Leo nimejifunika juu mpaka chini ili kujaribu kupata mwanaume wa kunitolea mahari. Si ni kujipanga,” Nyamu anasikika akizungumza katika video hiyo ambayo imesambazwa mitandoni.

Kwa maneno yake kwamba anavalia vizuri kwa heshima ili kumvutia mwanaume wa kumuoa kulizua maneno mengi mitandaoni huku baadhi wakijadili dhana ya ni kwa nini watu wengi wanadhani mwanamke mzuri wa kutulia kwenye ndoa ni yule anayevalia kiheshima nguo za kuficha maungo yake yote.

Wengine walimtania kwamba bado yeye ni mpenzi na mchumba wa polisi ambaye pia anajiongeza kama msanii wa Mugithi, Samidoh.

Ikumbukwe Karen Nyamu wamekuwa katika mahusiano ya muda mrefu na mpaka kupata watoto wawili ambapo ilidaiwa Nyamu alimchukua Samidoh kutoka kwa mkewe wa halali, Edday.

Miezi michache iliyopita wakati Nyamu bado hajazaa, walitupiana mikwara na Samidoh mitandaoni huku Nyamu akisema Samidoh hawezi kushrutishwa kumlea mtoto wao naye wakati Samidoh alidokeza maneno kwamab huenda hatokubali uzazi wa mtoto huyo aliyeuwa anatarajiwa.

Samidho aliachana na mkewe Edday wakati ambapo ilifahamika amempachika Nyamu mimba ya mtoto mwingine, baada ya awali kukiri na kuomba msamaha hadharani kwa mkewe kwamba kuwa na Nyamu ilikuwa makosa na hatorudia tena.

Kwa sasa, Nyamu anazidi kurindima ngoma za kampeni za Kenya Kwanza katika maeneo mbalimbali baada ya kutia kibindoni azma yake ya kuwania useneta Nairobi na badala yake kuamua kumuunga mkono aliyekuwa mbunge wa Starehe, Margret Wanjiru kutoka chama cha UDA.