"Mmoja akiku-bluetick mwingine anaomba namba, hatukai soko sana' Amber Ray ajigamba

Mwanamitindo huyo aliachana na Jimal Rohosafi mwishoni mwa mwaka jana, kisha akaingia mahusiano na IB Kabba ambaye pia waliachana wiki chache zilizopita.

Muhtasari

• Baada ya kuachana na Jimal Rohosafi, Amber Ray hakukawia kabla ya kumzindua Msierra Leone IB Kabba kama mchumba wake.

• Wiki chache baadae walitengana naye na akamuonesha mwanaume mwingine ambaye alisema ni mchumba wake mpya tena.

Mwanamitindo Amber Ray
Mwanamitindo Amber Ray
Image: Instagram//AmberRay

Mwanasosholaiti Amber Ray ameonekana kutupa bomu la moto kwa aliyekuwa mpenzi wake Jimal Rohosafi huku akionekana kufurahia maisha na mpenzi wake wa sasa ambaye alimtambulisha hivi majuzi kwenye mitandao yake ya kijamii.

Katika video ambayo Ray aliipakia kwenye Instagram yake akicheza densi ya mwendo pile, aliifuatisha kwa maneno yanayoonekana kumchooza Jimal kwa kusema kwamba alimkataa lakini akapata mtu mwingine wa kumsitiri.

“Mmoja akiku-bluetick mwingine anaomba namba yako. Mambo ni mengi masaa ndio machache. Hatukai sana kwa soko,” aliandika Amber Ray.

Wengi wametafsiri maneno hayo kwa njia tofauti tofauti huku wengine wakikisia huenda anamchokoza Jimal Rohosafi kwa hali yake ya sasa ambapo anajaribu kurudiana na aliyekuwa mke wake Amira, ila mkewe huyo amekataa katakata kama katibu kata wa kata ya Mkata aliyekataa kukata miti kabla ya mkate.

Mwezi Machi, Ray alipakia video kweney Instagram yake akionesha kuifuta tattoo ya Jimal aliyokuwa amechorwa mgongoni kama njia ya kumuonesha mapenzi. Hili lilifanyika baada ya wawili hao kutengana, muda mchache baada ya Jimal kuachana pia na mkewe wa kwanza Amira.

Kama ambavyo anasema kwamba hawakai kwa soko sana, Amber Ray kweli hakukawia sokoni kwani alikuja akapatana na bwana mmoja mkwasi kutoka taifa la Sierra Leone kwa jina Ib Kabba ambaye walisukuma maisha kwa wiki chache kabla ya kuachana na baadae tena Ray alizindua chuma kipya, mwanaume aliyesema ni mpenziwe na Kabba akasema anamjua kwani wakati wanachumbiana Ray alikuwa anamuambia mwanaume huyo ni rafiki tu.

Katika siku za hivi karibuni, Ray ameonekana kuyakubali maisha kwa maneno ambayo amekuwa akisema kwamba anajaribu kuishi maisha mazuri kwani kesho yake inategemea na jinsi atakavyojiweka katika maisha ya leo.

“Kila hatua unayofanya leo ina athari itakayodhihirika kesho. Leo ni malighafi ya siku zijazo! Leo ni nafasi yako ya kuzalisha yajayo unayotaka kuona, lakini utakuwaje na wakati ujao ikiwa huwezi hata kujitunza leo? Hivyo jivinjari mwenyewe ... na wakati unafanya! Fanya sawa! Fanya,” aliandika Amber Ray katika moja ya post zake.