(Video) Simple Boy amvisha pete mchumba mpya baada ya Madini Classic kuchukua Vishy

Wiki jana msanii Madini Classic alimtambulisha Pritty Vishy kwa wazazi wake, na wikendi Stevo akamvisha pete mchumba mpya.

Muhtasari

• Stevo Simple Boy na Pritty Vishy waliachana miezi kadhaa iliyopita kwa kile alituhumiwa kuchepuka na mwanamuziki kutoka pwani.

• Wiki jana Madini Classic na Vishy waliweka wazi kuwa wapenzi na kutambulishana kwa wana ukoo.

• Wikendi iliyopita Stevo alijibu mipigo kwa kumvisha pete mchumba wake mpya.

Ushindani baina ya msanii Stevo Simple Boy na aliyekuwa mchumba wake wa muda mrefu Pritty Vishy unaendelea. Licha ya wawili hao kuachana miezi michache iliyopita, kila mmoja anajaribu kadri ya uwezo wake kuidhihirishia dunia kwamab alikuwa bora zaidi kuliko mwingine.

Wikendi iliyopita, msanii Stevo Simple Boy alimvisha pete ya uchumba mpenzi wake mpya baada ya kuachana na Vishy, hii ilikuja wiki moja tu baada ya Vishy kuonekana kwenye video akitambulishwa kwa wazazi na anayedai kuwa mchumba wake mpya, mwanamuziki Madini Classic.

Simple Boy ambaye wikendi hiyo alikuwa anashehereheka kufikisha wafuasi laki moja kwenye akaunti yake mpya ya YouTube, miezi minne tangu kuifungua baada ya usimamizi wa awali kuipiga tanji ile ya kwanza, alipata baraka mara mbili baada ya kuenda kweney goti na kuomba posa kwa mchumba wake ambaye aliitikia na kukubali kuvishwa pete.

“Hayawi Hayawi Leo imekuwa siku nzuri imekuja sherehe yetu ndo tunaifungua na dua njema amebariki mwenyewezi waliokukataa watapa mastresi kwanza wale ma ex,” Stevo Simple Boy aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Wiki jana, Madini Classic alipakia rundo la picha kwenye Instagram yake akiwa pamoja na Pritty Vishy ambapo alisema ndiye mwenye bahati ya kumiliki chuma hicho kipya baada ya Stevo Simple Boy kubuma.

Simple Boy na Vishy walitengana miezi kadhaa iliyopita ambapo mwanamuziki huyo alikuwa anamtuhumu Vishy kwa kuchepuka na wanaume hamsini.

Vishy alikuja baadae akakubali kwamba aliwahi chepuka mara kadhaa wakati wanachumbiana na Stevo Simple Boy ila akakanusha vikali madai kwamba alichepuka na wanaume hamsini.

Alisema kwamba aliamua kuchepuka kwa sababu Simple Boy hakuwa anamkaribia kwani alikuwa anamuogopa. Simle Boy alisema ni ukweli hakuwahi mkaribia Vishy kwani yeye bado ni bikra.