"Alikiba alinituma niende kumpiga Diamond mawe" Kakake Alikiba, Issa Azam asema

Issa Azam kwa sasa anaambana na skendo dhidi yake kuwa shoga.

Muhtasari

• "Nikahama nikaenda kumtetea Platnumz, na kumwambia pita hapa, madini haya sio, watu hawa sio,” alieleza Issa Azam.

Kakake Alikiba, Issa Azam
Kakake Alikiba, Issa Azam
Image: IssaAZAM//iNSTAGRAM

Issa Azam, ambaye ni ndugu yake msanii mfalme wa Bongo Fleva Alikiba juzi alitumbuliwa na skendo na kuwa shoga na mwanaume mwingine, jambo ambalo amelikataa vikali mpaka kumwaga machozi hadharani mbele ya kamera za waandishi wa uhondo wa umbea.

Azam ambaye licha ya kuwa kaka wa Alikiba ambaye ni hasidi mkubwa kwenye gemu la muziki na msanii Diamond Platnumz, yeye aliamua kujitenga na ndugu yake na badala yake kuwa karibu na Diamond kama chawa wake.

Sasa amefichua na kuweka wazi kilichomtenganisha na ndugu yake na kuamua kumuunga mkono adui wake kimuziki.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi na vyombo vya habari baada ya mange Kimambi kusema kwamba licha ya kuwa na mke na familia, bado anatoka na mwanaume mwingine kwa jina Lampard kishoga, Azam alikana madai hayo na skendo kama hiyo iliwahi kumtokea ndugu yake, Alikiba mwaka 2012 na yeye ndiye alikuwa mstari wa mbele kuizima lakini kipindi hiki yamempata yeye Alikiba yupo kimya.

“Ali 2012 alipata skendo kama yangu sasa hivi, mimi ndio nilipata tabu Kariakoo kuizima. Kipindi hicho hamna Instagram, hamna nguvu kama sasa hivi, niliizima kila sehemu natembea kila makundi mitaani, ila Ali hajui,” alieleza Azam baian ya kwikwi kama mjane aliyefiwa mume kipindi cha fungate.

Vile vile, Issa Azam alidokeza kiini kilicholetqa tofauti kati yake na ndugu yake Alikiba na akaamua kumshabikia Diamond. Kulingana na yeye, Alikiba alimtaka kuenda kumpiga Diamond mawe katika tamasha lake alilokuwa ameliandaa.

“Na kwa nini nilimpenda Simba, ni baada ya shoo ya kwenda kumpiga Simba mawe. Nikaone haiwezekani mimi nihusike kumuumiza mtu, huu si mziki tena wa vita hii ya kuuana. Nikahama nikaenda kumtetea Platnumz, na kumwambia pita hapa, madini haya sio, watu hawa sio,” alieleza Issa Azam.

Issa kwa uchungu amesisitiza kuwa Skendo aliyozushiwa na mwanaharakati wa mitandaoni Mange Kimambi si ya kweli na kwamba imemuumiza sana na kumtaka Mange apost picha ambayo Issa yupo chumbani na Lampard ili anachokiongea Watu waamini.