"Pandeni miti mingi!" Kinaya cha maandishi kwenye lori lililobeba kuni

Wengine waliufananisha ujumbe huo kama ule wa nyani asiyeona kundule.

Muhtasari

• Maandishi kwenye gari lililobeba kuni likiwataka watu kupanda miti yalizua ghadhabu katika mitandao ya kijamii.

Lori la kubeba kuni
Lori la kubeba kuni
Image: Facebook

Picha ya lori ambalo lilikuwa limesheheni kuni hadi pomoni imezua utata mitandaoni baada ya lori hilo kuonekana na maandishi yanayowataka watu kuzidi kupanda miti kwa wingi.

Bila shaka picha hiyo imezua gumzo kwani inakuwa kama ni kinaya kikubwa kuwataka watu kuzidi kupanda miti kwa wingi huku gari lenyewe likiwa limebeba kuni amabzo zimetokana na miti hiyo.

Watu walionekana kuwa na maoni kinzani kuhsu hilo, baadhi wakihisi maandishi hayo ya kuwataka watu kuzidi kupanda miti hali ya kuwa wewe unaitumia kama kuni tena kujaza kwenye malori ni hatua inayoenda kinyume na masharti ya serukali yanayowataka watu kupanda miti kwa wingi ili kuboresha mazingira na kuzuia mabadiliko ya tabia ya nchi.

Kwa mfano nchini kenya, Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, Kenya inaendelea kukumbwa na hali ya mvua iliyochelewa na isiyo na uhakika. Ndiyo maana serikali na mamlaka zinazojihusisha na mazingira zimezidi kuwahimiza wakenya kunapanda miti ili kurejesha mandhari hii iliyoharibika, ili kupunguza hatari ya ukame na kuhimiza mvua zinazoendelea kunyesha katika eneo hili.

Nchini Kenya, mwishoni mwa mwezi Mei, Rais Uhuru Kenyatta alizindua kampeni ya kitaifa ya ukuaji wa miti kwa kasi na hakikisho la kujitolea kwa Kenya kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Alipokuwa akizungumza wakati wa uzinduzi katika mkutano wa rais kuhusu kampeni ya kitaifa ya ukuaji wa miti katika Ikulu ya Nairobi, Rais Kenyatta alisema kuwa hatua za ujasiri zinazochukuliwa na Serikali katika kuongeza misitu ya Kenya zinazaa matunda.

Katika kampeni ambazo zinaendelea kuhamasisha watu kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira kwa kupanda miti, kitu mtu anashauriwa kuhakikisha kila mwaka anapanda miti inayoendana na idadi ya miaka yake.