RIP! Msanii wa Bongo Fleva Ben Pol apoteza babake mzazi

Msanii huyo aliweka wazi kifo cha babake kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Muhtasari

• “Mungu Akutie Nguvu Katika Kipindi Hiki My Brother, Pole Sana,” Gozbert aliandika.

Msanii Ben Pol na babake
Msanii Ben Pol na babake
Image: Instagram//BenPol

Msanii wa miziki ya kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, Ben Pol ametangaza  kwamba amempoteza babake mzazi.

Akiweka wazi taarifa hizo za tanzia, Ben Pol amesema kwamba babake amefariki na kuwaacha katika upweke mkubwa.

Mastaa mbali mbali walifurika kweney ukurasa wake wa Instagram ambapo alipasua mbarika ya habari hizo za huzuni na kumpa pole.

“Ben, Pole sana Ndugu yangu. Allah akufanyie wewe na Familia yako wepesi kwenye kipindi hiki kigumu. Nakutumia kumbato la joto kipindi hiki chenye baridi mno kweney familia yenu,” aliandika mmoja kwa jina la Ecejay.

Pia msanii maarufu wa injili, Goodluck Gozbert ambaye waliwahi fanya kibao kimoja hatari pamoja kwa jina Mama alisikitishwa na kifo cha mzazi wa msanii huyo na kumpa pole.

“Mungu Akutie Nguvu Katika Kipindi Hiki My Brother, Pole Sana,” Gozbert aliandika.

Msanii Ben Pol alikuwa nchini Kenya wiki chache zilizopita katika kunadi mradi wa kutunza mazingira unaokwenda kwa jina Kijanisha ambapo alitembelea vituo mbali mbali vya habari na kufanya mahojiano ya kina kuhusu maisha yake kijumla.

Msanii huyo katika moja ya mahojiano ambayo Wakenya wengi walitaka kujua nini kilitokea katika mahusiano na ndoa yake na mjasiriamali na mrithi wa kampuni ya ya vileo ya Keroche, Anerlisa Muigai mpaka kumpelekea kubadilisha dini kutoka Ukristo hadi Uislam, Pol alisema kwamba hali ilikuwa ngumu na baada ya kutengana alipitia unyongovu mkubwa mpaka kumpelekea kutafuta huduma za mwanasaikolojia.

Pole sana Ben Pol kwa kumpoteza baba mzazi!