"Utapigwa teke na pundamilia ujifungulie mbinguni!" Nandy asutwa Twitter

“Mwishoe upigwe teke na pundamilia ujifungulie mbugani" - shabiki mmoja aliandika.

Muhtasari

• “Sasa wewe ukizalia hapo mbugani na mtoto akaliwa na hao pundamilia, Billnas atakuelewa kweli.?” - shabiki mwingine aling'aka.

Wachumba Nandy na Billnass
Wachumba Nandy na Billnass
Image: Nandy//Twitter

Msanii  wa kike wa Bongo Fleva, Nandy amejipata kuwa mwathirika wa hivi punde wa kuburuzwa kwenye mtandao wa Twitter baada ya kupakia video wakiwa na mumewe ambapo alionekana ameinama na kushikilia mgongo kama mtu anayeumwa tumbo huku wakiwa karibu na pundamilia katika mbuga moja nchini humo.

Katika picha hiyo, Nandy aliandika neno moja tu la ‘Maturity’ ambalo ni jina la albamu yake mpya inayotarajiwa kutoka hivi karibuni lakini watu wala hawakujali hilo, kilichowahusu zaidi ni kumburuza na kukejeli jinsi ambavyo alikuwa anaonesha ujauzito wake tena karibu na maeneo hatari ya mbuga ya wanyamapori.

Wengine wallionekana kumpa ushauri kwa njia ya kumzomea na kumtaka ajitulize nyumbani asubiri azae ndio hayo mengine ya kuzuru maeneo kama hayo yatakuja, huku baadhi wakihoji kwa mfano akatokea mnyama hatari kama simba, ataweza kukimbia na ujauzito wote ule ama ndio mwanzo anageuzwa kitoweo cha simba.

“Mwishoe upigwe teke na pundamilia ujifungulie mbugani, si ukitulize hicho kitumbo ndani kwani nani hajui kama uko na kibend bana,” mmoja kwa jina Julius aliandika kweney ukurasa huo wa Twitter.

“Halafu tuki comment mnasema tuna ukatili mtandaoni,” mwingine aliandika kuashiria kwamba watu wanaoburuzwa mitandaoni wanajitakia wenyewe.

“Sasa wewe ukizalia hapo mbugani na mtoto akaliwa na hao pundamilia, Billnas atakuelewa kweli.?” Mwingine kwa jina Jitu la Kale aliandika.

Japo kuwa mwanamuziki huyo anaonekana kabeba ujauzito uliokomaa kabisa lakini bado hajaamua kutulia na kusubiri itimie tisa kwani anazidi kujishughulisha katika mitikasi mbalimbali bila kujali kwamba atachoka au hata kumchosha mtoto tumboni.

Wikendi iliyopita, Nandy alifanay kufuru ya mwaka baada ya kuingia kwenye ukumbi na kumbuiza katika tamasha lake kubwa la kila mwaka almaarufu Nandy Festival licha kuonekana kalemewa na ujauzito.

“Huyo mtoto atazaliwa amechoka sana aisee,” shabiki mmoja kwa jina Kaka Jambazi alidakia kwa utani.

Nandy na Billnass walifunga harusi ya kifahari iliyotenga anga za Afrika mashariki wiki mbili zilizopita, miezi sita tu baada ya kuvishana pete za uchumba ambapo pia Billnass alilipa mahari ghali nyumbani kwao Nandy, kijijjini Mlandizi.