"Tuko duniani kwa wakati mzuri sio muda mrefu, jivinjari" - Zari Hassan

Zari alikuwa mke wa msanii Diamond Platnumz ambapo walizaa pamoja watoto wawili.

Muhtasari

• Zari alionekana kutetea hatua yake ya kuchumbiana na kijana aliyeonekana kuwa mdogo kiumri kumliko.

Mfanyibiashara na ambaye alikuwa mke wa msanii Diamond Platnumz, Zari Hassan
Mfanyibiashara na ambaye alikuwa mke wa msanii Diamond Platnumz, Zari Hassan
Image: Instagram//ZariHassan

Zari Hassan, mfanyibiashara mashahuri kutoka Uganda na ambayewengi katika ukanda wa Afrika Mashariki walimfahamu kutokana na mahusiano yake na mwanamuziki Diamond Platnumz, amekuwa akigonga vichwa vya habari hivi karibuni baada ya kuonekana akichumbiana hadharani na kijana mmoja ambaye ni mdogo mno kiumri kumliko.

Zari alijipata kuzungumziwa sana baada ya picha na video zake wakioneshana mahaba ya kijana huyo kuvuja na ilimbidi ajitokeze na kumtetea kijana huyo kwa kuweka wazi kwamab kinachosheheni umuhimu kwa sasa ni mapenzi yake na kijana wa watu na wala si maneno ya watu.

Zari sasa anasema kwamba katika maisha haya hatupo kuishi kwa muda mrefu na kuwataka watu yeyote anayetia bidi na jitihada katika maisha basi anastahili kujiliwaza kwa kujitunza vizuri kwani duniani tupo kwa ajili ya muda na nyakati nzuri na wala si kwa muda mrefu kama ambavyo wengi waansema.

“Ikiwa unafanya kazi kwa bidii, jivinajri kwa tafrija nzuri mwenyewe. Tuko hapa kwa wakati mzuri sio muda mrefu,” Zari alitoa ushauri.

Wengi walitafsiri ujumbe huu kwamba alimaanisha kujivinjari ni chaguo la mtu na kitu chochote anachokiona kinastahili kumpa tafrija ya moyo wake, na hivyo ni kama njia moja ya kuwasuta wale wanaomuwekea vikwazo na viwango vya watu anaofaa kuchumbiana nao.

Miaka kadhaa iliyopita, Zari alitengana na mwanamuziki Diamond Platnumz baada ya kuzaa na yeye watoto wawili ambapo alienda zake Afrika Kusini kuendesha biashara zake za ujasiriamali na mapema mwaka huu aliibuka tena baada ya kuonekana akishikana kimahaba na kijana mmoja mdogo aliyemtambulisha kwa jina GK Choppa.

Hawakudumu na yeye kwa muda mrefu kwani baada ya muda Zari alizifuta video na picha zote za pamoja na kijana huyo kwenye mtandao wake wa Instagram ambapo hivi majuzi tena ameonekana katika kichochoro kimoja jijini Dar es Salaam akiwa na huyo kijana mdogo ambaye inasemekana ndiye anayechumbiana naye kwa muda huu.

Licha ya kuonekana na vijaan hao dogo dogo, bado hilo halionekani kumsumbua baba watoto wake, Diamond Platnumz ambaye hivi majuzi alidokeza kwamba hana mpango wa kuingia kwenye ndoa hivi karibuni.