"Umaarufu wa kufanana na Wajackoyah umelemaza riziki yangu ya kila siku" - Gordon Owino

Mwendesha bodaboda huyo alisema biashara yake ya bodaboda haiendi tena kwani kila mtu sasa anamuona kama supastaa

Muhtasari

• “Huo umaarufu wa umma umeniathiriki pakubwa sana kwa sababu nilikuwa na watu ambao walikuwa wateja wangu wa bodaboda lakini sasa wananiona kama supastaa" - Owino.

• "Nimepoteza vitu vingi nimeporomoka kiuchumi au hata kifedha kwa sababu ya hilo,” Owino alisema.

Mwaniaji urais wakili msoni profesa George Wajackoyah na Gordon Owino, mhudumu wa bodaboda anayemfanana
Mwaniaji urais wakili msoni profesa George Wajackoyah na Gordon Owino, mhudumu wa bodaboda anayemfanana
Image: 2mbili tv

Gordon Owino, jamaa mwendesha boda boda amabye umaarufu wake umekuja baada ya kugu8ndulika kwamba anafanana na mgombea urais kwa chama cha Roots, wakili msomi George Wajackoyah amefunguka mengi jinsi amabvyo maisha yake yamebadilika tangu wimbi hilo la kumfananisha na Wajackoyah limkute.

Akizungumza kweney mahojiano ya kipekee na kituo kimoja cha habari ya mitandaoni humu nchini, Owino alisema kwamba umaarufu huo umeingilia kazi yake sana kwani tangu akutanishwe na Wajackoyah sasa kila mtu anamuona kama mtu maarufu ambaye ametajirika na hilo limelemaza kazi yake ya bodaboda.

“Huo umaarufu wa umma umeniathiriki pakubwa sana kwa sababu nilikuwa na watu ambao walikuwa wateja wangu wa bodaboda lakini sasa wananiona kama supastaa sana na badala ya kuabiri bodaboda niwapeleke, wao wanazingatia sana na huo umaarufu ambao niko nao, watu wanataka kupiga picha na mimi, wengine wanataka kunihoji, wengine wanataka nionekane kwenye chaneli zao, ni kitu kibaya na mwisho wa siku mimi mwenyewe huwa sipati faida. Nimepoteza vitu vingi nimeporomoka kiuchumi au hata kifedha kwa sababu ya hilo,” Owino alisema.

Alisema sasa watu popote aendapo wanamuona wanaanza kusema ndio huyo Wajackoyah na kuanza kumzingira jambao ambalo alisema si nzuri kwa upande wa riziki yake.

Mwendesha bodaboda huyo pia alisema imefikia mahali watu wanamuona wanaanza kumhusisha na bangi ambayo ndio ajenda kuu katika manifesto ya msomi wakili Wajackoyah. Alisema kwamba familia yake pamoja na yeye mwenyewe ni Wakristo walokole na hata siku moja katika maisha yake hajawahi kugusa au hata kuonja bangi lakini tu kutokana na mfanano wake na Wajackoyah basi watu wanamuona tu kama mtumizi wa dawa hiyo ya kulevya.

Wiki jana, mkuza maudhui wa YouTube, mchekeshaji 2mbili alimkutanisha na wakili msomi George Wajackoyah katika ofisi yake katika kile kilionekana kuwa ni mshangao mkubwa kwa mgombea huyo wa urais. Wajackoyah alifurahi kumuona Owino na akamkabidhi saa yake ghali ya mkononi pamoja na kiasi cha pesa.