(Video) "Mimi nimekuachia mama, nataka uniachie usingizi" Professor hamo amwambia mwanawe

Mwezi mmoja uliopita Hamo alipakia picha ya huyo mtoto na kusema kwamba wameongeza kura nyingine katika familia.

Muhtasari

• Mchana yote umeshinda ukilala, sisi tulikuwa kazini, tumekuja hapa wewe ndio umeamka.

Mchekeshaji Hamo the Professor hatimaye ameonesha sura ya mtoto wake mchanga kwa jamii ya wanamitandao huku akimgombanisha mtoto huyo kwamba hataki kulala hali ya kuwa ni usiku sana na wao wametoka kazini wamechoka.

Katika video hiyo aliyoipakia kwenye ukurasa wake wa Facebook, Hamo the Professor anaonekana akizungumza na mtoto huyo huku akidokeza kwamba ni saa tatu usiku na hata kumuahidi kwamba kwanzia leo amemuachia maziwa ya mamake.

“Ona sasa hivi ni saa ngapi, saa tatu usiku ndio umefungua hivi macho. Mchana yote umeshinda ukilala, sisi tulikuwa kazini, tumekuja hapa wewe ndio umeamka. Mimi nimekuachia mama, nimekuachia nyonyo. Mimi kitu nataka uniachie ni usingizi tu,” Hamo anaonekana akimzungumzia mtoto huyo mchanga asiyeelewa kama anazungumziwa.

Katika hali ya ucheshi wake wa kawaida, Hamo anaonekana akimbembeleza mtoto kumruhusu analale huku akimuambia kwamba yeye asubuhi huwa anarauka mapema alfajiri huku akimuacha amelala fofofo na kungoja jioni wakati wamerudi kutoka kazini wamechoka, mtoto ndio anaamka anataka wapige stori.

“Mimi nataka tu nilale kuliko ati sasa unataka tukae tuongee mpaka saa saba na asubuhi mimi nakuacha kama umezima. Sasa umekasirika, usikasirike, juu mimi nimeongea ukweli na ukweli unauma lakini hivyo ndio nimeshasema na hivyo ndio nakuomba wewe ulale leo mapema tafadhali utakuwa umenifanyia ihnsan,” Hamo anazidi kuzungumza na mwanawe huyo wa miezi kadhaa.

Tumeongeza kura nyingine ya wajackoyah Nani anajua kupiga ile ariririri nimpatie directions

Posted by Hamo The Proffessor on Tuesday, June 28, 2022

Miaka miwili iliyopita Hamo alijipata katika zogo la kumchafulia jina pakubwa baada ya mchekeshaji mwenza, Jemutai kumtuhumu hadharani kwamba wana watoto wawili pamoja lakini amewatelekeza licha ya Hamo kipindi hicho kuwa na kazi kama mtangazaji kwenye kituo kimoja cha redio nchini.

Sakata hilo lilitokota hata zaidi mpaka kuwapelekea wawili hao kuelekea hospitalini kutafuta huduma za msumbojeni yaani DNA ili kutambua kama kweli Hamo alikuwa baba mzazi na matokeo yakamuonesha kuwa baba wa kuwazaa watoto wale.

Hilo lilimdhalilisha sana moaka kuachishwa kazi katika redio ambapo muda mchache baadae alimuomba Jemutai msamaha hadharani na kuahidi kushirikiana kulea watoto wao pamoja licha ya kuwa na mke mwingine ambaye alikuwa anajulikana kihalali.