"Harmonize akiwa WCB alikuwa anavuta sana mpaka tunapigiwa simu na RC wa mkoa" - Sallam SK

Mendez aisema kwamab chanzo cha kunyamaziana na Harmonize ni hulka yake ya kuvuta moshi sana.

Muhtasari

• "Hata Tale alimuambia siku moja na yeye akamjibu, kwani sitohit, kwa hiyo usinifuatilie maisha yangu” Sallam SK alifunguka.

Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Meneja wa kazi za muziki za msanii namba moja wa muziki Afrika mashariki, Diamond Platnumz, Sallam SK amefunguka kiini cha uhasama wake na msanii Harmonize kutoka lebo ya Konde Music Worldwide.

Akizungumza katika kipindi chake cha Sallam Na, meneja huyo alisema kwamab hata katika msiba wa mke wa mbunge Babu Tale hawakusalimiana wala hata kuonana jicho kwa jicho na Harmonize kutokana na kile alisema mwanamuziki huyo anasemekana kutumia bangi ambayo bado ni haramu nchini humo.

Sallam Mendez alisema kwamab ugomvi baina yake na msanii Harmonize ilianza tu baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kipindi hicho, Paul Makonda kutaka Harmonize kufanyiwa vipimo vya kiafya kubaini kama kweli anatumia bangi au la, kutokana na alivyokuwa akionekana kwenye picha na video mitandaoni akiwa anaachia moshi mkubwa kutoka mdomoni kwa kile kinachoonekana ni uvutaji wa bangi au sigara.

Mendez alisema kwamba kuonekana kwa Harmonize akivuta moshi hata kabla ya kuondoka WCB kulifanya usimamizi wa lebo hiyo kuingia katika vita na mamlaka mbalimbali ambazo zilikuwa zinadai Wasafi inaficha wasanii wanaotumia bangi na hata kuonesha hadharani mitandaoni, jambo ambalo lilimfanya Sallam kujaribu kuzungumza na Harmonize lakini halikufua dafu.

“Tatizo lilianza toka simu ambazo tunapigiwa na viongozi kuambiwa Wasafi nyie ni kioo cha jamii, hio tabia ya Harmonize anatoa mamoshi na anaonesha wazi wazi sio tambia nzuri, nadhani kila kitu tulikuwa tunamuambia na kila kitu akawa anazungumza. Hata Tale alimuambia siku moja na yeye akamjibu, kwani sitohit, kwa hiyo usinifuatilie maisha yangu” Sallam SK alifunguka.

Harmonize aliondoka lebo ya Wasafi katika njia ya kishari mno huku baadae kukiibuka madai kwamba alikuwa ananyanyaswa kimapato kule kutokana na kazi zake za kimuziki, jambo ambalo mkubwa wake, Diamond Platnumz hakutaka kulizungumzia ila alipuuzilia mbali madai kama hayo ya kusema ni potovu ambayo yalikuwa yanalenga kuharibia Wasafi jina.

Miaka mitatu tangu kuondoka kwake Wasafi, Harmonize kwa sasa ni mmiliki wa lebo nyingine kubwa nchini humo ambapo amewapa mikataba wasanii chipukizi mbali mbali kama Ibraah, Anjella na wengine.